Hatua
ya Baby Madaha kuwa msanii wa kwanza mwanamke nchini Tanzania,
kujitokeza hadharani kumchambua msanii huyo mkubwa na mwenye heshma
kubwa ndani na nje ya nchi, imevuta hisia za wadau wa muziki nchini huku
akimwagiwa sifa kemkem kwa kujitokeza na kufuangua ufahamu wa wasichana
kutokana na imani kwamba Diamond ni mchawi anayetumia nyota za wanawake
kujipatia umaarufu.
Baby
madaha ambaye anatarajia kuzindua Single nne pamoja na muvi yake kali
zilizotengenezwa nje ya nchi, amesema kwamba kinachomkera zaidi ni
kitendo cha Diamond kudhalilisha wasicha wenzake kimapenzi, kila kukicha
kutoka na uwezo wake wa kifedha huku akitangaza wazi kwamba anafanya
mapenzi bila kutumia kondom kwa madai kwamba anatafuta mtoto.
"Tarehe
22 Jumapili Disemba mwaka huu pale Golden Tulip nitamuonyesha
Diamond,kuwa Queen of Swagg ni nani,ambapo yeye alizindua Single moja ya
ngololo pale Serena mimi ninazindua single 4 moja ikiwa ni Soundtrack
na Move yangu mpya ya the Galbladder, iliyonigarimu mamilioni
kuitengeneza nje ya nchi,huku show nzima ikidhaminiwa na Heinekein ambao
pia ndiyo wadhamini wa lebo ya Candy& candy ya jijini Nairobi, huku
mgeni rasmi akitarajiwa kuwa kiongozi mzito kutoka Ikulu ya Rais
Kikwete pale Magogoni jijini Dar es Salaam"alisema Baby Madaha.
Kuhusu
kauli yake kwamba Diamond ni mchawi alisema kwamba, "ingawa kuna maneno
mengi kwamba Diamond ni mchawi na kwamba anaweza kuniroga, mimi hilo
halinitishi kwa sababu yeye anashindana na wanawake badala ya kushindana
na wanaume wenzake, katika maendeleo ila ukweli ni kwamba mimi si
shindani na wanwake kwa sababu ni marafiki zangu, ila ninashindana na
wanaume katika suala la maendeleo na siamini katika uchawi na akiona
kwamba anaweza kuniroga kama ambavyo watu wake wananitangazia
ajaribu,kwani mimi ninazungukwa na nguvu za Mungu na si Nguvu na Mganga
wa kienyeji".
Baby
Madaha alisema kwamba baada ya kumwangusha nyota huyo wa muziki nchini
na kumfanya afikirie kumroga katika uzinduzi huo ataanza kufanya ziara
nchini nzima kuitangaza Queen of Swagg itakayozidi kuipoteza ngololo ya
Diamond katika ramani ya muziki ndani na nje ya nchi, kabla ya kuendelea
na show kali sehemu mbalimbali Dunaini kama ilivyo pangwa na
wanadhamini wkake wakuu Heinekein.