Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

BASI LA CHAMPION LAPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI 29 KATIKA MLIMA CHIMWAGA LIKITOKEA CHUO KIKUU DODOMA (UDOM)



Gari lenye namba za usajili T 704 ADR  aina ya Scania bus la kampuni ya CHAMPION.

Gari lenye namba za usajili T 704 ADR  aina ya Scania bus la kampuni ya CHAMPION likiendeshwa na dereva ALLY RAMADHANI, mnyaturu, umri kati ya  35 - 40, mkazi wa Kisasa Dodoma likiwa limebeba wanamichezo/wanavyuo wa vyuo vikuu vya Zanzibar na State University Zanzibar likitokea chuo kikuu Dodoma (UDOM) likielekea kituo kikuu cha mabasi Dodoma lilipinduka na kusababisha majeraha kwa abiria wapatao 43 kati yao Majeruhi  29   waliotibiwa na kuruhusiwa  na majeruhi 14 wamelazwa katika Hospitali ya  Rufaa ya Mkoa Dodoma, wote wakiwa ni wanaume.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamishna msaidizi wa Polisi SUZAN S. KAGANDA amesema ajali hiyo imetokea tarehe 15/12/2013 majira ya saa 06:15 hrs huko eneo la mlima wa Chimwaga UDOM      Kata ya  Makulu Dodoma mjini.
Kamanda KAGANDA amewataja majeruhi katika ajali hiyo ambao ni:-
1.     Hamisi Hamisi, miaka 28, mshirazi, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
2.     Bashiru Yusuph, miaka 26, sukuma, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
3.     Abdallah Juma, miaka 28, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word namba 1.
4.     Ally Sharifu, miaka 24, mshirazi, mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
5.     Mussa Mkanga, miaka 21, mzanzibari, Mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
6.     Seifu Fakii juma, miaka 27, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word 1
7.     Ahamed Mohamed Hassani, miaka 23, Mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 11.
8.     Richard Mwasonga, miaka 36, mnyiha, Tingo wa bus, Miyuji Dodoma. Amelazwa word namba 1.
9.     Juma Nasoro, miaka 23, mshirazi, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.
10.                        Hemedi Mohamed, miaka 29, Mzanzibari, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.

11.                        Mussa Mtaugana, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar  University
12.                        Adam Mwale Bonifasi, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University.
13.                        Amelazwa word namba 1.
14.                        Mohamed Ally Mohamed, miaka 23, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University.
15.                        Nassoro Mohamed Saidi, miaka 25 -30, mwanachuo State University Zanzibar. Hali yake si nzuri sana na amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
 
Aidha Kamanda KAGANDA amesema Chanzo cha ajali ni  mteremko mkali wenye kona iliyosababisha dereva kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha ajali ya gari kupinduka upande wa kulia na kulala kiubavu. Mara baada ya ajali hiyo dereva alikimbia kwenda kusikojulikana na juhudi za kusaka dereva huyo zinaendelea. Pia  uchunguzi unaendelea kubaini iwapo gari hilo lilikuwa na tatizo lolote.
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma linatoa Wito kwa madereva kila mara wawe makini barabarani hasa kipindi hiki cha mvua na kuwa makini hususani kwa barabara zenye milima.
Read more >>

MAHAFALI YA 19 YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI DAR ES SALAAM (DSJ)‏‎

Mahafali ya 19 ya chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) yamefanyika ijumaa ya desemba 13 mwaka huu ambapo wahitimu katika ngazi za stashahada na cheti kwenye fani ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma, na mahuasiano ya umma wamehitimu.
Tazama picha za baadhi ya matukio wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
 Mgeni  rasmi akiwa katika meza kuu  na Mkuu wa chuo , pamoja na viongozi wengine wa chuo na viongozi wa Serikali ya wanafunzi 
 Kutoka kushoto ni Fabian, Dotto Mandolin Kahindi, Abushehe Nondo, Benjamin Mwangoka
  Wahitimu wakiwa katika mahafali hayo 

Rais Mstaafu wa DASJOSO Alfred Ochali akisoma risala
 Mkuu wa Chuo cha DSJ, Joachim Rupepo akitoa hotuba yake na kumkaribisha mgeni rasmi kutoa nasaha zake (P.T)

Mgeni Rasmi Bi. Jimhada malembeka akitoa nasaha  kwa niaba ya Meya wa manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa
 
 Wahitimu wakiwa wanasikiliza kwa umakini hotuba kutoka kwa mgeni rasmi
Kutoka kushoto ni  Anifa, Grace, Zourha na Cartace ambao pia walikuwa wahitimu katika mahafali hayo
Wahitimu wakiwa wanatunukiwa
Wahitimu wakiwa wanatoa mkono wa Shukurani baada ya kutunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali

Wahitimu wakiwa katika pozi baada ya kumaliza mahafali
Baadhi ya wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu zao
Kutoka kushoto ni Elizabeth Lazaro akiwa na Jackline  Marandu ambao pia ni wahitimu.
 Wageni waalikwa wakiwa wanafuatilia kwa makini kinacho endelea katika mahafali hayo 
 Kwaito time
 
Read more >>

BREAKING NEWZZZZZZ!!!: AJALI YATOKEA DARAJA LA MLALAKUWA, MIKOCHENI JIJINI DAR



Ajali imetokea leo asubuhi kawe Darajani Dar ambapo gari hiyo Inayoonekana kuharibika vibaya ilitumbukia katika mto huo na kusababisha kifo cha Mtu mmoja ambaye anaonekana akielea juu ya maji.
Read more >>

DU!.. AJALI NYINGINE HII YAUA WAWILI AKIWEMO DEREVA WAWILI...!



Hii kati ya ajali ambazo zimekuwa zikitokea kila mara Tanzania
WATU
wawili wamekufa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya basi
waliolokuwa wakisafiria la Simiyu Express kupinduka katika eneo la
Ihumwa nje kidogo ya manispaa ya Dodoma. Basi hilo lenye namba za usajili T 717 ANL aina ya scania basi lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Mramba Issa (31). Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Susan Kaganda, alisema kuwa basi hilo lilikuwa linatokea Bariadi kwenda Dar es salaam likiwa na abiria 60 liliacha njia na
kupinduka kutokana na mwendo kasi . Kamanda alisema kwamba ajali hiyo ilitokea leo alfajiri majira ya saa tisa usiku katika barabara ya Dodoma-Dar es salaam eneo la Elshadai . Kamanda Kaganda aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni
pamoja na dereva wa basi hilo Mramba Issa mkazi wa Magomeni
Dar es salaam na Frola Erenest(21) Mwalimu wa shule ya msingi Mwamoto
kolokolo, Bariadi. Aidha kamanda akizungumzia zaidi ajali hiyo alisema kwamba basi hilo lilikuwa likiwakwepa askari wa barabarani kwa kupita njia za panya. Alifafanua kuwa kwa basi hilo kusafiri usiku huo ni kukwepa askari . Aliwataka pia wamiliki wa magari kuweka madereva wawili kwa
magari ya masafa marefu na pia wazingatie sheria za barabarani.

Read more >>

FAMILIA YA MAREHEMU DKT MVUNGI YAWASAMEHE WALIOMUUA..! SOMA ZAIDI HAPA



Familia ya marehemu Dk Edmund Sengondo Mvungi pamoja na chama cha NCCR-Mageuzi kimewasamehe wale wote waliohusika na kumuua Dkt Mvungi ambaye alikuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba

Rai hiyo imetolewa na msemaji wa familia ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James francis Mbatia wakati wa ibaada maalum ya kumwombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam

Mbatia amesema Tangu marehemu Dkt Mvungi alipopata tazito la kuvamiwa na watu waliomkata mapanga Novemba 3 mwaka huu hadi mauti yalipompata Novemba 12, yamesemwa maneno mengi, lakini wao kama familia na chama wameamua kuwasamehe wauaji wote

"Tunasema kwamba tumewasamehe, damu ya Dkt Mvungi imeshamwagika, alikuwa mpigania nchiniwe na katiba mpya, sasa amekufa lakini tunafurahi kuona mchakato wa katiba mpya unaendelea na ndiyo ilikuwa dhamira yake"alisema Mbatia

Dkt Mvungi alivamiwa na kukatwa mapanga nyumbani kwake Kibamba jijini dar es salaam hali iliyopelekea kifo chake wakati akipatiwa matibabu nchini Afrika kusini novemba 12 mwaka huu.
Credit:edwinmoshi.com
Read more >>

Waziri wa Nishati na Madini akutana na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuzungumzia Masuala ya Gasi

unnamed_3d3fb.jpg
Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Profesa Sospeter Muhongo,Baadhi ya Wajumbe kutoka Benki ya Dunia wakichangia taarifa iliyowasilishwa kuhusu masuala ya Gasi wakati wa kikao baina yao
unnamed_1_539c6.jpg
Bw. Albert Zeufack Mtaalamu toka Benki ya Dunia akiwasilisha taarifa ya kuhusu Masuala ya Gasi
unnamed_2_7faaf.jpg
Kamishna Msaidizi anayesimamia masuala ya Gasi Asilia Engineer Nobert Kahyoza akitoa ufafanuzi wakati wa kikao hicho
unnamed_3_eb8ec.jpg
Kamishna Msaidizi anayesimamia Maendeleo ya Nishati Bw. James Andikile akisisitiz ... hicho katikati ni Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo
Picha na ( Asteria Muhozya - Nishati na Madini)(P.T)
Read more >>

NAOMBENI RADHI KWA PICHA HIZI JAMANI: MWANAMKE MMOJA AMWAGIWA MAJI YA MOTO NA MWANAMKE MWENZIE KISA WIVU WA KIMAPENZI...! CHEKI PICHA ZA TUKIO HAPA


Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. 


Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.  

Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

Na Gadiola Emanuel -Arusha

Mwanamke mmoja mkazi wa Mbuguni Arusha,Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kisa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.
Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru alikolazwa,Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma lililopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka afike nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kumwagia maji ya moto.Neema Teti-Majeruhi
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la madaktari hospitalini hapo. Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru Hospitali Bi.Neema Bayo amesema matukio kama hayo yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali
nchini,bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini
Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha Maria Maswa akizungumza wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika hospitali ya mount Meru,amesema yanapotokea matukio hayo,walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo hayo.Maria Maswa-Afisa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa.
Read more >>

AJALI: WATU 41 KIWEMO WAZIRI MKUU EDWARD LOWASSA WANUSURIKA KIFO BAADA YA NDEGE WALIYOPANDA KUPASUKA MATAIRI..! SOMA ZAIDI HAPA



Abiria 37 na wafanyakazi 4 wa ndege ya Precision Air wamenusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wamepanda kupasuka matairi wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha leo majira ya mchana.

Waziri mkuu mstaafu ambaye ni mbunge wa Monduli, Edward Lowassa alikuwa miongoni mwa abiria wa ndege hiyo waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha.
Shirika la ndege la Precision Air limetoa tamko rasmi kwa umma, ambapo limeeleza kuwa watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wako salama.

Read more >>

MULTICHOCIE TANZANIA YAFUNGA MWAKA KWA KUSHEREHEKEA NA WANAHABARI, WADAU JIJINI DAR

Baadhi ya wadau na wanahabari wakijiachia wakati wa sherehe ya kufunga mwaka ya kampuni ya Multichoice Tanzania jana usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Hawa wakiserebuka kwa muziki.
Wanahabari na wageni wengine waalikwa wakijisevia msosi wakati wa sherehe hiyo ndani ya Serena Hotel.
Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally (wa kwanza kushoto) na Mhariri wa gazeti la Championi Ijumaa John Joseph (wa kwanza kulia) wakichukua msosi katika sherehe hiyo.
Saleh na John wakibadilishana mawazo.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiwa katika sherehe hiyo.
Burudani zikiendelea ndani ya ukumbi wa hoteli ya Serena, Posta jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Multichoice Tanzania jana usiku ilisherehekea kufunga mwaka 2013 na wanahabari pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha kumaliza mwaka kwa mafanikio. Katika sherehe hiyo waalikwa walijumuika katika kucheza muziki, kupata vinywaji na vyakula pamoja ikiwa ni shukrani kutoka kwa kampuni hiyo.
(PICHA: GPL)
Read more >>

Serikali, Tume ya Uchaguzi wavutana........

Lukuvi_a4895.jpg
Na Raymond Kaminyoge, Mwananchi
Wakati Serikali ikisema Daftari la Kudumu la Wapigakura litaboreshwa kwa ajili ya kura za maoni ya Katiba Mpya, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema haina mpango huo kwa sababu muda uliobaki ni mfupi.
Badala yake Nec imesema inajiandaa kuboresha daftari hilo kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili kuingiza wale wote waliotimiza miaka 18 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema jana kwamba itakuwa vigumu kuliboresha daftari hilo kwa ajili ya upigaji wa kura za maoni utakaofanyika mwanzoni mwa mwaka 2014 kwa sababu muda uliobaki ni mfupi na hakuna fedha za kufanya hivyo.(E.L)

"Muda uliobaki kwa ajili ya upigaji wa kura za maoni ni mfupi, itakuwa vigumu kwa tume kuliboresha daftari la wapigakura nchi nzima ila tunajiandaa kuliboresha kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015," alisema Jaji Lubuva.
Alisema nchi ni kubwa kijiografia kiasi kwamba unahitajika muda mrefu kwa ajili ya kuliboresha daftari hilo na kwa vile zoezi la upigaji kura za maoni litafanyika mwanzoni mwa 2014, tume itakuwa imechelewa kufanya hivyo.
Kauli ya Serikali
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alipoulizwa jana mjini Dodoma kuhusu tamko la Jaji Lubuva, alisema msimamo uliotolewa na Waziri Mkuu wiki iliyopita ndio msimamo wa Serikali.
"Serikali tunajiandaa, na wao (NEC) wanajua fedha za mwanzo tumeshapeleka na mchakato umeanza. Wameshakagua mashine zitakazotumika....process (mchakato) hii yote inalenga kura ya maoni," alisema Lukuvi.
Hata hivyo, Lukuvi alisema inawezekana kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba Katiba Mpya itapatikana Aprili 26, mwaka huu ndiyo inayowachanganya, wanaona muda uliopo ni mfupi lakini hilo ni la Serikali na siyo tume.
Desemba 5, mwaka huu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alivihakikishia vyama vya siasa na Watanzania kwamba Daftari la Kudumu la Wapigakura litaboreshwa kabla ya upigaji kura ya maoni juu ya Katiba Mpya. Hali kadhalika Pinda alisema Serikali itatumia daftari hilo la Nec katika upigaji kura ya maoni ya katiba kwa pande zote za Muungano.
Pinda alitoa kauli hiyo wakati akihitimisha hotuba yake ya Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni wa mwaka 2013 ambapo suala la daftari la wapiga kura lilibua mvutano mkali. Wabunge wa Tanzania Bara walitaka daftari la wapiga kura liboreshwe kwanza, huku wale wa Zanzibar wakitaka wasio na vitambulisho vya ukaazi waruhusiwe kupiga kura kwa kutumia daftari la Nec
Pinda alisema daftari la kudumu la Nec kwa sasa lina orodha ya Watanzania wa Bara wanaoishi Zanzibar, lakini hawawezi kupiga kura kwenye uchaguzi ule wa ndani wa upande wa Zanzibar.
Uboreshaji Daftari
Mara ya mwisho daftari hilo kuboreshwa ilikuwa mwaka 2010 na sasa kuna idadi kubwa ya vijana waliofikisha umri wa miaka 18 ambao wanatakiwa kuwemo kwenye daftari hilo.
Sifa ya kupiga kura ya maoni ni mtu kuwa mwananchi kuandikishwa kwenye daftari hilo.
Uhuru wa Tume
Kuhusu uhuru wa tume hiyo, Jaji Lubuva alisema yeye na makamishna wa tume wako huru na hawaingiliwi na chombo chochote cha Serikali wala chama cha siasa katika kutekeleza majukumu yake.
"Haijawahi kutokea hata siku moja kwamba tume imeagizwa na kiongozi yeyote wa juu kuendesha uchaguzi kwa kupendelea chama au mgombea," alisema.
Alisema tume inafanya kazi zake kwa uhuru lakini kama wananchi wanataka mabadiliko yoyote kwenye Katiba Mpya kuhusu namna ya kupata tume, hilo ni suala la msingi. "Tume iko huru, ila wananchi wanaweza kuamua namna ya kupata Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo wanapenda iwe, sisi hatuna kipingamizi," alisema Jaji Lubuva.
Kauli za wanasiasa
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema kauli ya Nec inaashiria kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilidanganya Bunge na Watanzania wakati wa mjadala wa Muswada wa Kura ya Maoni kuwa daftari litaboreshwa kabla ya upigaji wa kura za maoni. Alisema kauli hiyo inaashiria kwamba wananchi waliopoteza kadi, waliokosa fursa wakati wa uboreshaji mwaka 2010 na waliofikisha umri wa kupiga kura watakoseshwa haki ya kupiga kura kuamua hatima ya nchi yao.
Mnyika alisema Nec imeamua kung'ang'ania daftari lenye kasoro ambalo limekuwa likilalamikiwa tangu mwaka 2010 kwamba linahitaji kuhakikiwa.
Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba alipotafutwa jana kuzungumzia hilo, simu yake ilikuwa ikiita bila majibu, kama ilivyokuwa kwa James Mbatia wa NCCR-Mageuzi
Read more >>

BALOZI SEFUE AZINDUA TIMU YA WATAALAMU WAZALENDO WA SEKTA YA MALIASILI

1 db8e0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizindua Timu ya Wataalamu wa Tanzania wa Kushughulikia Mkataba wa Maliasili.
2 6ee4f
Profesa Paul Collier Mtaalamu wa Msuala ya Uchumi na Sera wa Kimataifa akiwawasilisha mada.
3 2aeac
Baadhi ya Washiriki wa Hafla ya Uzinduzi wakimsikiliza Profesa Paul Collier(kulia).
4 82a8f
Mkuu wa Utafiti na Sera kutoka Taasisi ya UONGOZI, Dennis Rweyemamu akiwasilisha mada juu ya Programu ya Mkataba wa Maliasili za Tanzania.(P.T)
5 98211
Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania Filiberto Cerian Sebregondi akiuliza swali kwa wawasilishaji mada.
6 8285f
Mwakilishi wa Benki ya Dunia Dk. Albert Zeufack akichangia mada.
7 1e136
Baadhi ya washiriki hafla hiyo.
8 24847
Baadhi ya washiriki hafla hiyo.
9 ed49c
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) akizungumza jambo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Alexandre Leveque.Kushoto ni Mwenyekiti wa Timu ya Wataalamu wa Tanzania wa Kushughulikia Mkataba wa Maliasili, Profesa Luoga Florency.
10 b6b91
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akitoa taarifa fupi kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baada ya kuzindua timu hiyo.Kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mku wa Taasisi ya UONGOZI, Profesa Joseph Semboja.
Picha zote na Hussein Makame
Read more >>

Sarafu moja kuchochea ukuaji wa uchumi Afrika Mashariki............

sarafuclip_7289e.jpg
Na George Njogopa, Mwananchi
Wengi wanaitazama hatua iliyochukuliwa na viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya kuridhia kuanzishwa kwa sarafu ya pamoja ni sawa na kusukuma tofali kwenye kina kirefu cha maji bila kuwa na matarajio ya kulifikia tena tofali hilo.
Kwa mujibu wa malengo ya jumuiya hiyo, kufikia mwaka 2023 mataifa yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakuwa yamefikia shabaha ya kuwa na sarafu moja hatua ambayo itafungua uwanja mpya wa ushirikiano wenye nguzo tatu.(E.L
).
Kukamilika kwa shabaha hiyo kutategemea pia utashi wa kisiasa kutoka kwa nchi wanachama bila kujali idadi ya raia wake.
Iwapo shabaha hiyo itafanikiwa kama ilivyopangwa basi Kanda ya Afrika Mashariki itakuwa imeingia kwenye rekodi mpya kwa kuwa itakuwa Jumuiya ya pili kuwa na sarafu moja ya fedha ikitanguliwa na ile ya Umoja wa Ulaya.
Juhudi kama hizo za kuwa na safaru za pamoja zimewahi kufanywa na nchi zilizoko kwenye ushirikiano wa kibiashara kwa nchi za Asia ya mbali, lakini hazikuzaa matunda.
Mkataba wa Umoja wa Ulaya unaojulikana kama 'Maastricht Treaty' ulisainiwa kwa mara ya kwanza Februari 7, mwaka 1992 na baada ya kupita mwaka mmoja utekelezaji wake ulianza kazi. Umoja huu ulitimiza miaka mingine saba kutimiza ndoto ya sarafu moja 'euro'.
Kwa kuzingatia biashara ya kubadilishana fedha na mtiririko wa biashara katika masoko ya kimataifa, sarafu ya euro inatajwa kuwa ni miongoni mwa sarafu zilipata mafanikio makubwa kwa kipindi kifupi baada ya kuanzishwa. Inasadikika baadaye huenda sarafu hiyo ikawa na nguvu katika soko la kimataifa.
Maktaba
Mkataba wa kuanzishwa kwa sarafu moja kwa nchi za Afrika Mashariki umesiniwa ikiwa imepita miaka 21 tangu kuasisiwa kwa mkataba wa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya. Pamoja na hatua hiyo iliyoanzishwa na viongozi wa Afrika Mashariki inatazamwa ikiwa ni sawa na kutosa tofali kwenye kina kirefu, lakini wanauchumi wanaona kwamba ni wazo linalokaribiana na ukweli.
Mbali na hayo kugundulika kwa rasilimali ghafi katika baadhi ya mataifa, ni moja ya vigezo vinavyofanikisha ndoto ya kuwa na sarafu moja. Kimsingi sarafu ya pamoja inaziwajibisha nchi wanchama kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na kudhibiti kuporomoka kwa uchumi.
Eneo la Afrika Mashariki ambalo linakadiriwa kuwa na idadi ya watu wanaofikia milioni 135 lina uwezo wa kuzalisha bidhaa zitakazohimili ushindani wa kimataifa. Tanzania pekee ambayo kwa sasa ipo kwenye hatua za mwisho za kuchimba gesi na mafuta ina uwezo wa kuvutia wawekezaji wa moja kwa moja na kuzika kasumba ya miaka mingi ya utegemezi wa misaada kutoka mataifa yenye nguvu ya kigeni.
Iwapo mradi unaozinduliwa na Kenya wa ujenzi wa reli kwa msaada wa Serikali ya China utakamilika kwa wakati, mafuta yaliyogunduliwa hivi karibuni nchini Uganda na Kenya-utavutia wawekezaji wengi wa kigeni na kutoa msukumo mpya wa kibiashara miongoni mwa nchi wanachama. Reli hiyo itapitia katika baadhi ya nchi wanachama.
Akizungumzia mipango ya maendeleo kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mtaalamu wa masuala ya uchumi, Christoper Mbiku anasema wazo lolote la kuunganisha nguvu na kuwa na sarafu moja litasaidia kusukuma mbele kasi ya ukuaji uchumi.
Anasema iwapo ndoto hiyo itatimia kwa wakati basi pato jumla ukuaji uchumi wa ndani kwa nchi wanachama litakuwa limefikia wastani wa dola 85 bilioni za Marekani. Hata hivyo, mtaalamu huyo anaonya kuhusu hali ngumu zinazoweza kujitokeza iwapo mamlaka husika zitashindwa kufanya mapinduzi sera zake za fedha.
"Suala la kuwa na sarafu moja kwa maoni yangu ni suala lisilokwepeka kwa ajili ya mustakabali wa jumuiya hii, lakini kuna changamoto nyingi ambazo lazima zitafutiwe ufumbuzi kabla ya kufika mwisho.
"Hili suala linahitaji muda na pia lazima sera zote za uchumi na sheria za nchi zipitiwe upya ili kwenda na mahitaji yaliyoko kwenye mkataba wa Jumuiya, vinginevyo tutajikuta tukijuta mbele ya safari" anasema mtaalamu huyo.
Kwa upande mwingine, wataalamu wa uchumi na siasa za kimataifa wanaona kuwa nchi zilizoko kwenye jumuiya hiyo zina nafasi kubwa ya kupiga hatua kama zitaendelea kutilia mkazo haja ya kuimarisha sera za kiuchumi na kuboresha miundombinu yake.
Kuna hali ya matumaini inayoanza kuchomoza ndani ya jumuiya hiyo hasa kutokana na hatua ya hivi karibuni ya kuanzishwa kwa mifumo inayofanana kuhusu masula ya fedha na bajeti za nchi. Kwa mara ya pili mfulilizo nchi hizo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zimekuwa zikisoma bajeti zake kwa wakati mmoja kila ifikapo mwezi Juni.
Safari ya mafanikio
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye pia mwenyekiti wa Jumuiya hiyo anasema safari ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio, sasa imeanza.
" Kwa hakika tumeanza kupiga hatua kusonga mbele. Tunaamini kuwa iko siku tutafika kule tunakokusudia na kufurahia matunda yetu. Kuanzishwa kwa soko la pamoja, ushuru wa forodha na mpango huu wa sarafu ya pamoja kutasaidia kupunguza gharama kubwa kwa wananchi wetu," anasema Rais Uhuru.
Kabla ya nchi wanachama kuingia kwenye sarafu ya pamoja kwanza zitawajibika kubainisha hali yake ya uchumi na namna zitakavyodhibiti mfumuko wa bei. Pia kutaundwa chombo maalumu kitachojulikana kama Benki Kuu kwa ajili ya kushughulikia mzunguko wa fedha.
Read more >>

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA TAIFA HUDUMA ZA FEDHA NCHINI.

unnamed_b8eb0.jpg
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Prof. Benno Ndulu, akisaini mfano wa cheti cha Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la kusimamia na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Wanaoshuhudia nyuma (katikati) ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kulia kwake ni Malkia Maxima wa Uholanzi (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha Sada Mkuya Salumu. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
unnamed_1_f8844.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha, wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
unnamed_2_f4dcc.jpg
Malkia Maxima wa Uholanzi, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa Changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Mohammed Gharib Bilal imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
unnamed_3_4f844.jpg
Malikia Maxima wa Uholanzi, akibofya kitufe kama ishara ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR(P.T)
unnamed_4_fddc4.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Malkia Maxima wa Uholanzi na Naibu Waziri wa Fedha, Sada Mkuya Salumu, wakiwa wameshikilia Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha baada ya kuzinduliwa leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania. Picha na OMR
unnamed_5_728f9.jpg
unnamed_6_bf214.jpg
Baadhi ya wadau wa Sekta za Fedha waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia, wakati wa uzinduzi.
Read more >>

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger