Showing posts with label WASANII. Show all posts
Showing posts with label WASANII. Show all posts

LULU MICHAEL AJIBU TUHUMU ZA KUFUMANIWA AKINANII NA YOUNG DEE KWENYE GARI...HIKI NDICHO ALICHOKISEMA

MWISHONI mwa wiki iliyopita, taarifa zilienea katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari Bongo kwamba msanii wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young Dee’ na nyota wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wamebambwa na polisi wa doria wakivunja amri ya sita ndani ya gari aina ya Hyundai, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tukio lililojaa utata mkubwa. 

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao walinaswa wakifanya uchafu huo na askari waliokuwa doria lakini wakawavuta chobingo na baada ya muda, wakawaachia na kutokomea kusikojulikana.
Ili kupata ukweli wa tukio hilo la aibu, paparazi wetu alianza kwa kumvutia waya Young Dee na kumsomea mashtaka yake ambapo alifunguka kuwa ni kweli amezisikia habari hizo lakini akakana kwamba ishu hiyo siyo ya kweli bali imezushwa na kundi la watu wenye lengo la kumharibia jina lake mbele ya jamii.
 
David Genzi ‘Young Dee’.
“Siyo kweli kabisa, isitoshe nina kama mwezi mzima sijaonana na huyo Lulu, huku ni kutaka kuchafuliana majina tu,” alisema Young D.

Habari zinadai kuwa licha ya Young Dee kukanusha kuwa hajaonana na Lulu kwa muda mrefu, siku ya tukio walikuwa pamoja ingawa hawakutaka kuonekana na mtu yeyote.

Kwa upande wa Lulu alipotafutwa, alifunguka: “Kweli nimesikia ishu kama hiyo ila kinachonishangaza na kunisikitisha ni kwamba siku hiyo ya tukio inayotajwa mimi nilikuwa nyumbani na siku nzima sikutoka kwenda popote, hata hiyo Mbezi iliyotajwa mimi siielewi kabisa, hata lile gari mimi sina gari la aina hiyo wala sijawahi hata kulipanda gari hilo na huyo Young Dee nina muda mrefu sana sijaonana naye,”

“Usiku wa kuamkia leo nilimpigia mtangazaji mmoja ambaye aliirusha habari hiyo redioni, nikataka kujua ameipata wapi habari hiyo? Akanijibu kwamba amepata tetesi tu. Sasa kama ni tetesi kwa nini asichunguze kabla hajanichafulia jina?”

“Pia alisema kuna askari wa doria walitukamata, nikamtaka anipeleke hicho kituo cha polisi tulikopelekwa ili tuthibitishe kama ni kweli maana ishu hii inanichafua mimi na familia yangu, akashindwa kufanya hivyo.
“Yaani naomba ieleweke kuwa sijafumaniwa na siwezi kufumaniwa na mtu kama Young Dee maana  kwanza hata sijawahi kukutana naye hivi karibuni, sipendi kuchafuliwa na haya yote namuachia Mungu atawajibu wote wanaonizushia,” alisema Lulu.
Read more >>

BABY MADAHA AKOLEA KIMAHABA NA MENEJA WAKE


 STAA wa filamu Bongo anayetamba na ngoma yake ya Summer Holiday amesema kuwa kutokana na mahaba mazito anayopatiwa na mwandani wake Joe Kariuki ambaye ni Meneja wake hafikirii kumuacha kamwe.
 
Akistorika na paparazi wetu alisema, tangu aanze uhusiano na pedeshee huyo anayemiliki studio ya Candy n’ Candy  nchini Kenya, amekuwa akijiona mwenye fahari kubwa kwenye sayari ya mapenzi kutokana na upendo anaomuonesha na kumfanya asiwaze kumpotezea kamwe.
“Kusema kweli huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi lakini abadani sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na uhusiano naye ila porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo natamani niamie Kenya ili tuwe karibu wakati wote,”alisema Baby Madaha.
Aliongeza kuwa kikubwa kilichompelekea kuwa naye ni kutokana na upendo wake wa kweli alionao kwake siyo kutokana na suala la mkwanja kama wengi wanavyodhani.
Read more >>

BABY MADAHA ABAINI HILA ZA DIAMOND PLATNUMZ........ATOBOA SIRI NZITO ILIYOJIFICHA

Msanii wa muziki wakizazi kipya nchini Tanzania Baby Madaha katika poz
 
Hatua ya Baby Madaha kuwa msanii wa kwanza mwanamke nchini Tanzania, kujitokeza hadharani kumchambua msanii huyo mkubwa na mwenye heshma kubwa ndani na nje ya nchi, imevuta hisia za wadau wa muziki nchini huku akimwagiwa sifa kemkem kwa kujitokeza na kufuangua ufahamu wa wasichana kutokana na imani kwamba Diamond ni mchawi anayetumia nyota za wanawake kujipatia umaarufu.
Baby madaha ambaye anatarajia kuzindua Single nne pamoja na muvi yake kali zilizotengenezwa nje ya nchi, amesema kwamba kinachomkera zaidi ni kitendo cha Diamond kudhalilisha wasicha wenzake kimapenzi, kila kukicha kutoka na uwezo wake wa kifedha huku akitangaza wazi kwamba anafanya mapenzi bila kutumia kondom kwa madai kwamba anatafuta mtoto.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania,Baby Madaha akiwa katika poz,
Akizungumza na Habarimpya.com Baby Madaha alisema kwamba,uzinduzi wa kazi yake itafanyika katika Hotel ya Golden Tulip ambapo atatumia uzinduzi huo kumwonyesha Diamond kwamba wanawake si chombo cha starehe kama anavyo fikiria, huku akimwonyesha kwamba yeye ni Queen Of Swagg (QOS), na kwamba staili hiyo itafunika staili ya ngololo ya single moja iliyobeba uchafu wa ngono na uchawi ndani ya Album yake iliyozinduliwa katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
"Tarehe 22 Jumapili Disemba mwaka huu pale Golden Tulip nitamuonyesha Diamond,kuwa Queen of Swagg ni nani,ambapo yeye alizindua Single moja ya ngololo pale Serena mimi ninazindua single 4 moja ikiwa ni Soundtrack na Move yangu mpya ya the Galbladder, iliyonigarimu mamilioni kuitengeneza nje ya nchi,huku show nzima ikidhaminiwa na Heinekein ambao pia ndiyo wadhamini wa lebo ya Candy& candy ya jijini Nairobi, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa kiongozi mzito kutoka Ikulu ya Rais Kikwete pale Magogoni jijini Dar es Salaam"alisema Baby Madaha.
Kuhusu kauli yake kwamba Diamond ni mchawi alisema kwamba, "ingawa kuna maneno mengi kwamba Diamond ni mchawi na kwamba anaweza kuniroga, mimi hilo halinitishi kwa sababu yeye anashindana na wanawake badala ya kushindana na wanaume wenzake, katika maendeleo ila ukweli ni kwamba mimi si shindani na wanwake kwa sababu ni marafiki zangu, ila ninashindana na wanaume katika suala la maendeleo na siamini katika uchawi na akiona kwamba anaweza kuniroga kama ambavyo watu wake wananitangazia ajaribu,kwani mimi ninazungukwa na nguvu za Mungu na si Nguvu na Mganga wa kienyeji".
Baby Madaha alisema kwamba baada ya kumwangusha nyota huyo wa muziki nchini na kumfanya afikirie kumroga katika uzinduzi huo ataanza kufanya ziara nchini nzima kuitangaza Queen of Swagg itakayozidi kuipoteza ngololo ya Diamond katika ramani ya muziki ndani na nje ya nchi, kabla ya kuendelea na show kali sehemu mbalimbali Dunaini kama ilivyo pangwa na wanadhamini wkake wakuu Heinekein.
Read more >>

SINTAH APIGA PICHA ZA MITEGO KISHA KUZIACHIA MTANDAONI....CHEKI HAPA




Tuekuwa tukimzoea Sintah kutusaidia kufunguka au kuwapa makavu wale wadada wote wanaokuwa wanaacha maungo yao nje na kuweka picha katika mitandao ya kijamii.., Unapomnyooshea kidole kimoja mwenzako unasahau kama vidole vinne vinakuangalia ww, basi sinta alilisahau ilo. tazama picha 3 hapo chini kisha ufunguke Sintah anafaa kukosoa wenzake au na yeye ni wale wale watafuta kiki??


Read more >>

Wyclef Jean awasili Lagos nigeria tayari kuwa MC show ambayo Vanessa Mdee atatumbuiza pamoja na wakali wengine wa Nigeria

Vanessa Mdee aka Vee Monoey ndiye msanii pekee wa Tanzania ambaye amepata nafasi ya kutumbuiza katika show kubwa nchini Nigeria ya ‘Rythm Unplugged 2013’ ambayo inatarajiwa kufanyika kesho na host wa show hiyo atakuwa msanii wa Marekani Wyclef Jean.
Wyclef Jean in nigeria Wyclef baada ya kuwasili Naija
Wyclef Jean tayari amewasili nchini humo kwa ajili ya show hiyo kubwa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka, na kuhusisha wasanii wakubwa wa Naija wakiwemo P-Square, Wiz Kid, Davido, D’Banj na wengine.
Wyclef Jean in lagos
Jean alitweet masaa machache kabla hajaondoka Marekani, “I am on my way to Africa today !v “Nigeria” “Ghana” We all Love Nelson Mandela! Then I will be in Jamaica my second home performing at “sting”.
Hii ni mara ya pili kwa Wyclef kwenda Nigeria kuhost tamasha la muziki, baada ya ile ya MTV Africa Music Awards.
Read more >>

AIBU: LULU MICHAEL NA YOUNG D WAFUMWA LIVE WAKIFANYA MAPENZI KWENYE GARI....!



Jana kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha Clouds FM chini ya bwana Sudi Brown ama Gossip Cop kulikuwa na fununu kali iliyokuwa inamuhusu mwanadada wa Bongo Movies na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Young D 'Young Dar es Salaam' kama mwenyewe anavyojiita baada ya wawili hao kukutwa kwenye gari wakifanya lile tendo linaloruhusiwa kufanywa mara baada ya mdada na mkaka kufunga ndoa.
                                   Young D
Kwa mujibu wa Sudi Brown 'Gossip Cop' wawili hao walikutwa maeneo ya Mbezi Beach ndani ya gari aina ya Hyundai ya mwanadada Lulu na polisi wa doria wakivunja amri hiyo iliyokatazwa na vitabu vyote vitakatifu kwa maana ya biblia, Quran na vitabu vingine vya dini ulimwenguni.

Habari zainasema baada ya wawili hao kukutwa eneo hilo na polisi walipelekwa pembeni gizani na kuongea na Polisi kabla ya wao kutokomea wasipojulikana na gari hilo.

Alipopigiwa simu mwanadada LULU alipokea na kukata muda mfupi na baadaye Young D alipopigiwa simu alitoa majiu ya utata kama alivyoongea mwenyewe kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha Clouds Fm.

MSIKILIZE MWENYEWE HAPA
Read more >>

PICHA: Rich Mavoko atoa machozi kwa Mama Sharo Milionea anayedai kutopewa Mahali za Mwanae

Hitmaker wa Roho Yangu Rich Mavoko amemtembelea mama mzazi wa marehemu Sharo Milionea huko Muheza Tanga. Mavoko amepost picha hii akiwa na mama mzazi wa msanii huyo aliyefariki Novemba mwaka jana inayoonesha akiwa kwenye simanzi zito kutokana na alichokuwa akisimuliwa na mama huyo.

 Huu ndio ujumbe wa Rich Mavoko aliyouandika baada ya kusimuliwa na mama huyo.

 "Muda mwingine wasanii tunahitaji tukumbuke wenzetu walio tangulia tena kwa kuwa enzi ata kwa kuwatembelea ndugu zake coz kuna vitu vinauma sana ukielezewa hapa alikuwa ana nielezea sharo baada ya kufa haki zake nyingi hajui zipo zinaenda wapi na mambo mengi yanayo muhusu marehem sharo kiukweli ili niuma... pole sana mama angu binadamu ndivyo walivyo,” ameandika Mavoko.
Read more >>

CHUCHU AJICHORA TATUU YA RAY, RAY NAE AJIBU!



KATIKA hali inayoonesha kuna kitu kikubwa kinakuja mbeleni, msanii wa filamu, Chuchu Hans amejichora ‘tatuu’ inayosomeka kwa jina la Ray huku anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ naye akiwa amejichora tatuu inayosomeka kwa jina la Chuchu.

Ray na Chuchu.
Picha ambazo gazeti hili limezinasa zinawaonesha wawili hao wakipigia ‘promo’ uhusiano wao huku wadau wengi wakiyafananisha mapenzi yao na ya njiwa.
Ili kujua undani juu ya jambo hilo, mwandishi wetu aliwatafuta wasanii hao ambapo Chuchu alionekana kukerwa na swali hilo na kujibu kwa ufupi kuwa hataki kusumbuliwa.
“Hivi hamchoki kufuatilia maisha ya watu jamani? Naomba mniache,” alisema Chuchu Hans.
Kwa upande wa Ray, simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
GPL:
Read more >>

MASTER JAY AFUNGUKA NA KUSEMA WASANII WA BONGO FLAVA NI WEZI


Producer mkongwe na C.E.O wa MJ Records Master J amesema kuwa wasanii wa Tanzania wanawaibia watayarishaji wa muziki.

“Huwezi kuchukua wazo langu uende kulitumia kutengeneza hela halafu uniambie kwamba ‘bwana mimi sikupi kitu’, wasanii ni wezi tu Bongo.” Amesema Master J.

Unaweza kudhani labda aliteleza kidogo kusema hilo, lakini kwa kuwa ana uhakika na anachokisema, producer huyo mwenye mchango mkubwa kwa muziki wa kizazi kipya hapa nchini aliweka mkazo kwenye maneno yake.

“Watu wanaogopa kuongea, mimi ngoja niongee tu ukweli, wasanii wa Bongo ni wezi. Kitu wanachokifanya ni wizi. Unajua mwizi anakaaga kimya, lakini wanakwenda kwenye media wanaropoka ‘nimeingiza million 300 (kwa kutumikia haki ya Lamar bure na simpi kitu)’. Yaani unaiba halafu unaenda unatangaza kwenye media!” alifunguka Master J.

“Hata hawaogopi! Walivyokuwa hawajui kwamba sheria hairuhusu kufanya hivyo, na kiukweli akiamua kupania anapata cha kwake, sema tu maproducer hawafuatilii. Lakini wanavunja sheria kabisa na ni wezi. Huwezi kufanya hivyo halafu unaenda unatangaza, kaa kimya…kula na kipofu. Sio sawa wanavyofanya.” Aliongeza kwa msisitizo.
Read more >>

BAADA YA KUSINGIZIWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA BRAZIL ASHA BUI AONEKANA SALOON SINZA....

Mwigizaji wa filamu za kibongo aliyesemekana kuwa amekatwa nchini brazil akiwa na madawa ya kulevya Aisha Bui ameonekana nchini hivi karibuni akiwa kwenye salooni ya mwanadada mwingine muigizaji Nisha iliyopo maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.

 
Mwadada huyo ambaye tayari ameigiza filamu kadhaa na mastaa wenzake alionekana kwenye saloon ya Salma Jabu(Nisha) akiwekwa sawa nywele zake kama anavyoonekana pichani.
Read more >>

MUONEKANO MPYA WA AGNES MASOGANGE TAZAMA PICHA ALIZOWEKA INSTAGRAM

Pichani juu ni taswira za mpya za Video Queen wa Bongo, Agness Gerald 'Masogange' alizotupia kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Read more >>

PICHA ZA DAYNA AKIBAMBIWA NA NJEMBA UFUKWENI WAKIFANYA YAO HADHARANI BILA AIBU!





Read more >>

BINT MACHOZI LADY JAY DEE AZIDI KUTISHA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI



Ule usemi wa ukubwa dawa,umezaa matunda kwa mwanamuziki wa bongo fleva nchini, Lady jaydee aka Anaconda, baada ya kuwa ndiye mwanamuziki pekee nchini Tanzania anayeongoza kuwa na mashabiki wengi kwenye mtandao wa kijamii wa FACEBOOk. 

Lady jaydee amefikisha FANS 150,956 hadi sasa akifuatiwa na Mtangazaji wa clouds fm mwenye kipaji cha kipekee na sauti yenye mvuto, Millard ayo ambaye yeye amejizolea ma Fans 150,653 huku namba tatu ikiwa imeshikilwa na mkali mwenyewe aka mfalme wa bongo fleva naseeb abdul au Diamond ambaye amejizoelewa ma Fans 138,471 hadi sasa kwenye mtandao huo wa kijamii wa FACEBOOK, hii inazidi kuonyesha ni jinsi gani lady jaydee anavyokubalika na kuungwa mkono na jamii katika kazi yake ya muziki,, BiG up kwa sana#TEAM ANACONDA

Read more >>

PRODYUZA: WEMA ALITAKA NIWE KUWADI

Na Stori: Shakoor Jongo
BAADA  ya kudaiwa kufanya ngono katika magari ya Kampuni ya Endless Fame inayoongozwa na Wema Issac Sepetu, Prodyuza, Rashid Mohammed ‘Chid Classic’ amefunguka na kusema chanzo cha yote ni mshahara  na ukuwadi ndani ya kampuni hiyo wala siyo uzinzi, Amani linakujuza.
Prodyuza Rashid Mohammed ‘Chid Classic’.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, Chid amesema hajafukuzwa katika kampuni hiyo kama alivyodai mratibu wa kampuni hiyo, Petit Man bali ameondoka baada ya kuchoka  kufanya kazi bila ya kulipwa mshahara.
“Ni uongo kusema kwamba nimenaswa nikifanya uzinzi Coco Beach nikiwa ndani ya magari ya Wema, sijawahi hata siku moja kufanya hivyo kwani nina kwangu ambako nina uwezo wa kumwingiza mwanamke wakati wowote,” alisema.
Wema Isaac Sepetu.
“Tangu kampuni ianzishwe haijawahi kulipa mishahara unadhani nitakuwa na moyo wa kufanya kazi, sikwenda pale kufanya ukuwadi kama wengine, tena nawaomba wasiendelee kusema uongo kwani nina mengi nayajua ya Endless Fame,” aliongeza Chid.
Baada ya kusikia maelezo hayo, Amani lilimtafuta Wema bila ya mafanikio ndipo likaongea na meneja wake, Martin Kadinda.
“Nina wasiwasi na kauli za Chid kwanza tatizo siyo mshahara na hayo masuala ya ukuwadi ni uongo na uzushi, kama ni kweli kwa nini asiongee siku zote hadi lilipoibuka hili la kunaswa akifanya uzinzi kwenye gari?” alihoji Kadinda.
Read more >>

HII NDIO ZAWADI YA MSANII HUYU WA P SQUARE ALIYOMPATIA MKE WAKE..!!

 







Msanii huyo Peter Okoye alimtumia mke wake hivi karibuni Zawadi zenye thamani kubwa sana ikiwemo Pete ya Diamond na Range Rover Sports ya mwaka 2013

Read more >>

hizi ndizo sababu za kwanini wanaume kibao wanapenda kumshobokea jokate mwegelo!


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhuRvR8dky0QxS0qcweZzQrH5ozyJbVEhbBljMkjt-LExmyQI91WpRMjs6pi1rvlSa0_yMOMqwufHqY2UrDqTo7KKHg14iE_R74gCRAd9R1ubIT8LI0IY4ep9OEYA_ITIg9L95Uvophy8E/s1600/DSC_5108.jpgMrembo anayefanya vizuri katika mambo mengi sana nchini Jokate Mwegelo amezungumza na kutaja Mambo manne yanayomfanya apendwe sana na wanaume wengi hapa nchini. 
1. Kujiamini
Hii ndi sababu kubwa ya kwanza aliyoitaja jokate. Ansema hamna kitu kinachowavutia watu, hasa wananume kama kujiamini. Mwanaume anapenda msichana anayejiamini. Zaidi ya yote hamna kitu kinachosema kuwa “I’m sexy” Zaidi ya mwanamke anayejiamini
 
2. Kujitegemea
Hii ni kama sababu ya kwanza hapo juu,  Jokate anasema hamna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vya kwako basi jua atakupenda sana
 
3. Kupendeza
Jokate anasema ni muhimu kwa wadada kuvaa nguo nzuri ambazo zitakupendeza kulingana na mwili wako hasa hasa nguo zenye rangi ya kuonekana.
 
4. Tabasamu
Tabasamu kila saa kwani tabasamu linakufanya unaonekana mzuri Zaidi.
Read more >>

Mzee SMALL Awalaani wanaomzushia Kifo...!!

Msanii mkongwe wa vichekesho Said Ngamba almaarufu kama Mzee Small, amemlaani mtu aliyetoa taarifa za uongo kuwa amefariki dunia jana usiku.


Akizungumza na tovuti ya Bongo5 waliomtembelea nyumbani kwake Tabata Mawenzi leo asubuhi, Small amesema alipatwa na mshituko baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu wanasambaza taarifa kuwa amefariki dunia, na kumlaani mtu aliyosambaza taarifa hizo za uongo.
Kwanza nawashukuru (Watanzania) na nawaheshimu kunipigia simu na kumtafuta mchawi, maana yake nyinyi ndiyo mumemvumbua mchawi,nawashukuru Radio zote,Tv zote nazishukuru mimi mzima bado nipo hai” Alisema Mzee huyo mcheshi.
Kwanza mke wangu alishituka alafu mimi mwenyewe nilikuwa nimelala, lakini kwakweli mimi nilijisikia vibaya, namalaani huyo mtu,namlaani kwanzia leo mpaka kiama na mwenyezi mungu atamuona na kumsikia” Alisema Mzee Small.
Naye mke wa Mzee Small amesema kwa upande wake ameathirika kwa kiasi fulani kwakuwa yeye ni muuguzi mkuu, alihitaji kuulizwa maendeleo ya Mzee Small kabla ya kutangaza taarifa za uongo.
Mimi ni mke wa Mzee Small kwakweli kwa tukio lililotokea limeniumiza sana kwasababu mimi ndiyo muuguzaji mkuu wa huyu bwana,niko nae inakuwa vigumu jambo kama hili linapotokea wakati mimi sijui chochote, kwakweli limeniumiza. Nawaomba Watanzania tufike mahala tuangalie, tusianze kusambaza vitu ambavyo hatuka ukweli navyo” Alisema mke wa Small.
Read more >>

TAZAMA PICHA ALIYOWEKA BEYONCE AKIWA AMESHIKILIA BANGI NA POMBE KWA WAKATI MMOJA


beyonce
Mama wa Blue Ivy na mke wa Rapper Jay Z, Beyonce Knowlence Carter aliwashangaza mashabiki na wapenzi wa kazi zake za kimziki hivi karibuni kupitia mtandao wa kijamii wa Tumblr. Beyonce akiwa na marafiki zake na dada yake Solange amabaye ni mwanamuziki pia, walikuwa  katika matembezi ya mapumziko huko nchini Jamaica, Beyounce alipost picha ambayo ameonekana akiwa ameshikilia mkono mmoja bia na mkono mwingine kitu kama msokoto wa bangi …
beyonce-weed-09122013
Wakati dada yake na rafiki zake wakijachia na bia huku wakidandia miti, Beyonce alikuwa amepozi na chupa ya bia na kitu kama bangi. Picha hiyo imezua mjadala kwa mashabiki kwamba mwana mama huyo anatumia mmea huo wa kijamaica.
Read more >>

"Natamani nipate Mimba Jamani".....LINAH

STAA wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ juzikati ameweka wazi nia yake ya kusaka mtoto, Risasi Mchanganyiko linakushushia.
Estelina Sanga ‘Linah’.
 
Akizungumza na  mwandishi wetu Desemba 9, mwaka huu jijini Dar, Linah alisema tangu alipoingia kwenye muziki hakuwahi kufikiria kushika ujauzito kwa kuwa alikuwa bado hajajiandaa kufanya hivyo.
Nyota huyo ambaye aliwahi kuzama  katika penzi zito la  staa mwenzake, Amin Mwinyimkuu alisema kuwa kwa sasa hali ni tofauti na anataka kuzaa iwapo atashika ujauzito.
Nilipokuwa  katika uhusiano wangu wa kwanza hakuna hata siku moja niliyohisi kama nitakuja kutamani kupata mtoto maana mwenzangu aliponiambia tuzae nilimkatalia tofauti na leo hii natamani nishike mimba na ulimwengu wote ujue kwamba nina mimba,” alisema Linah.
Hata hivyo Linah alikwepa kuweka wazi uhusiano wake wa sasa na hakutaka kumwongelea Amin.

Read more >>

Huu Ndio Mwonekano mpya wa Msanii RAY C Akionyesha Mapaja yake...!!

Mwanadada RAY C katika Pozi la kimahaba


 
Read more >>

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger