RATIBA YA MAKUNDI UEFA HII HAPA ,ARSENAL MDOMONI MWA WAKALI BAYERN MUNCHEN

Bbml7UbIgAAQdUV_fa774.jpg
Read more >>
widgets for blogger

HIZI NDIO MBINU ZA KUONGEZA MVUTO KWA MPENZI WAKO... SOMA ZAIDI HAPA


KAMA WEWE BADO HUJAJIUNGA NASI, UNAWEZA KUJIUNGA HAPA MOJA KWA MOJA ONLINE <<<BOFYA HAPA NA LIKE PAGE YETU>> : 


Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka.

Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida – mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?
Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.
Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO
Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO
Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.
Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.
Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI
Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.
Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!
Read more >>

HIZI NDIZO PICHA KALI ZA YALIYIJIRI WEEKEND HII, AFTER SKUL BASH ILIVYOHAPEN:




KAMA WEWE BADO HUJAJIUNGA NASI, UNAWEZA KUJIUNGA HAPA MOJA KWA MOJA ONLINE <<<BOFYA HAPA NA LIKE PAGE YETU>> : 

 
 
 Mashabiki kibao wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri jukwaani 
 
 Baadhi ya wasanii chipukizi kutoka anga ya muziki wa Bongofleva pia walipewa nafasi ya kuonesha umahiri wao wa kulishambulia jukwaa vilivyo.
 
 
 Watangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu na Dj Fetty wakijadiliana jambo nyuma ya jukwaa.
 
 
 

 
 Mashabiki wakifurahi burudani iliyokuwa ikitolewa juu ya steji
 
 
 DJ Mahiri kutoka Clouds FM akifanya makamuzi ya nguvu ndani ya Mbalamwezi Beach,wakati wa tamasha la After Skull Bash likiendelea,Tamasha hilo limewakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali.
 
 
 Msanii Nguli wa muziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda a.k.a Mtoto wa Mama Said akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar. 
 
 
 Mmoja wa watangazaji mahiri wa Clouds FM,Hamis Mandi a.k.a B Dozen akitoa utaratibu mzima wa tamasha hilo utakavyofanyika.Tamasha hilo limeratibiwa na Clouds FM kwa kushirikiana na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd.
 
 
 Msanii wa muziki wa Kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga ya muziki wa bongofleva,Rich Mavoko akikamua vilivyo jioni ya leo kwenye tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.
 
 
Mashabiki waliofika kwenye tamasha hilo wakifuatilia kwa makini.
Read more >>

LULU MICHAEL AJIBU TUHUMU ZA KUFUMANIWA AKINANII NA YOUNG DEE KWENYE GARI...HIKI NDICHO ALICHOKISEMA

MWISHONI mwa wiki iliyopita, taarifa zilienea katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari Bongo kwamba msanii wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young Dee’ na nyota wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wamebambwa na polisi wa doria wakivunja amri ya sita ndani ya gari aina ya Hyundai, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tukio lililojaa utata mkubwa. 

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao walinaswa wakifanya uchafu huo na askari waliokuwa doria lakini wakawavuta chobingo na baada ya muda, wakawaachia na kutokomea kusikojulikana.
Ili kupata ukweli wa tukio hilo la aibu, paparazi wetu alianza kwa kumvutia waya Young Dee na kumsomea mashtaka yake ambapo alifunguka kuwa ni kweli amezisikia habari hizo lakini akakana kwamba ishu hiyo siyo ya kweli bali imezushwa na kundi la watu wenye lengo la kumharibia jina lake mbele ya jamii.
 
David Genzi ‘Young Dee’.
“Siyo kweli kabisa, isitoshe nina kama mwezi mzima sijaonana na huyo Lulu, huku ni kutaka kuchafuliana majina tu,” alisema Young D.

Habari zinadai kuwa licha ya Young Dee kukanusha kuwa hajaonana na Lulu kwa muda mrefu, siku ya tukio walikuwa pamoja ingawa hawakutaka kuonekana na mtu yeyote.

Kwa upande wa Lulu alipotafutwa, alifunguka: “Kweli nimesikia ishu kama hiyo ila kinachonishangaza na kunisikitisha ni kwamba siku hiyo ya tukio inayotajwa mimi nilikuwa nyumbani na siku nzima sikutoka kwenda popote, hata hiyo Mbezi iliyotajwa mimi siielewi kabisa, hata lile gari mimi sina gari la aina hiyo wala sijawahi hata kulipanda gari hilo na huyo Young Dee nina muda mrefu sana sijaonana naye,”

“Usiku wa kuamkia leo nilimpigia mtangazaji mmoja ambaye aliirusha habari hiyo redioni, nikataka kujua ameipata wapi habari hiyo? Akanijibu kwamba amepata tetesi tu. Sasa kama ni tetesi kwa nini asichunguze kabla hajanichafulia jina?”

“Pia alisema kuna askari wa doria walitukamata, nikamtaka anipeleke hicho kituo cha polisi tulikopelekwa ili tuthibitishe kama ni kweli maana ishu hii inanichafua mimi na familia yangu, akashindwa kufanya hivyo.
“Yaani naomba ieleweke kuwa sijafumaniwa na siwezi kufumaniwa na mtu kama Young Dee maana  kwanza hata sijawahi kukutana naye hivi karibuni, sipendi kuchafuliwa na haya yote namuachia Mungu atawajibu wote wanaonizushia,” alisema Lulu.
Read more >>

WWE!! :TAZAMA PICHA 25 JIINSI JOHN CENA ALIVYOCHEZEA KICHAPO KITAKATIFU TOKA KWA RANDY ORTON:









































RANDY ORTON AMESHINDA MIKANDA MIWILI YA WWE BAADA YA KUMSHINDA JOHN CENA KWENYE Tables, Ladders & Chairs Match,AMBAPO JOHN CENA ALISHINDWA KUTETEA TAJI LAKE MOJA LA WWE HIVYO KUPELEKEA RANDY KUNYAKUA MATAJI YOTE MAWILI YA UZITO WAJUU NA KUWEKA HISTORIA.
Read more >>

BABY MADAHA AKOLEA KIMAHABA NA MENEJA WAKE


 STAA wa filamu Bongo anayetamba na ngoma yake ya Summer Holiday amesema kuwa kutokana na mahaba mazito anayopatiwa na mwandani wake Joe Kariuki ambaye ni Meneja wake hafikirii kumuacha kamwe.
 
Akistorika na paparazi wetu alisema, tangu aanze uhusiano na pedeshee huyo anayemiliki studio ya Candy n’ Candy  nchini Kenya, amekuwa akijiona mwenye fahari kubwa kwenye sayari ya mapenzi kutokana na upendo anaomuonesha na kumfanya asiwaze kumpotezea kamwe.
“Kusema kweli huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi lakini abadani sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na uhusiano naye ila porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo natamani niamie Kenya ili tuwe karibu wakati wote,”alisema Baby Madaha.
Aliongeza kuwa kikubwa kilichompelekea kuwa naye ni kutokana na upendo wake wa kweli alionao kwake siyo kutokana na suala la mkwanja kama wengi wanavyodhani.
Read more >>

BASI LA CHAMPION LAPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI 29 KATIKA MLIMA CHIMWAGA LIKITOKEA CHUO KIKUU DODOMA (UDOM)



Gari lenye namba za usajili T 704 ADR  aina ya Scania bus la kampuni ya CHAMPION.

Gari lenye namba za usajili T 704 ADR  aina ya Scania bus la kampuni ya CHAMPION likiendeshwa na dereva ALLY RAMADHANI, mnyaturu, umri kati ya  35 - 40, mkazi wa Kisasa Dodoma likiwa limebeba wanamichezo/wanavyuo wa vyuo vikuu vya Zanzibar na State University Zanzibar likitokea chuo kikuu Dodoma (UDOM) likielekea kituo kikuu cha mabasi Dodoma lilipinduka na kusababisha majeraha kwa abiria wapatao 43 kati yao Majeruhi  29   waliotibiwa na kuruhusiwa  na majeruhi 14 wamelazwa katika Hospitali ya  Rufaa ya Mkoa Dodoma, wote wakiwa ni wanaume.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamishna msaidizi wa Polisi SUZAN S. KAGANDA amesema ajali hiyo imetokea tarehe 15/12/2013 majira ya saa 06:15 hrs huko eneo la mlima wa Chimwaga UDOM      Kata ya  Makulu Dodoma mjini.
Kamanda KAGANDA amewataja majeruhi katika ajali hiyo ambao ni:-
1.     Hamisi Hamisi, miaka 28, mshirazi, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
2.     Bashiru Yusuph, miaka 26, sukuma, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
3.     Abdallah Juma, miaka 28, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word namba 1.
4.     Ally Sharifu, miaka 24, mshirazi, mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
5.     Mussa Mkanga, miaka 21, mzanzibari, Mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
6.     Seifu Fakii juma, miaka 27, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word 1
7.     Ahamed Mohamed Hassani, miaka 23, Mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 11.
8.     Richard Mwasonga, miaka 36, mnyiha, Tingo wa bus, Miyuji Dodoma. Amelazwa word namba 1.
9.     Juma Nasoro, miaka 23, mshirazi, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.
10.                        Hemedi Mohamed, miaka 29, Mzanzibari, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.

11.                        Mussa Mtaugana, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar  University
12.                        Adam Mwale Bonifasi, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University.
13.                        Amelazwa word namba 1.
14.                        Mohamed Ally Mohamed, miaka 23, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University.
15.                        Nassoro Mohamed Saidi, miaka 25 -30, mwanachuo State University Zanzibar. Hali yake si nzuri sana na amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
 
Aidha Kamanda KAGANDA amesema Chanzo cha ajali ni  mteremko mkali wenye kona iliyosababisha dereva kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha ajali ya gari kupinduka upande wa kulia na kulala kiubavu. Mara baada ya ajali hiyo dereva alikimbia kwenda kusikojulikana na juhudi za kusaka dereva huyo zinaendelea. Pia  uchunguzi unaendelea kubaini iwapo gari hilo lilikuwa na tatizo lolote.
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma linatoa Wito kwa madereva kila mara wawe makini barabarani hasa kipindi hiki cha mvua na kuwa makini hususani kwa barabara zenye milima.
Read more >>

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger