YANGA YATOA RASMI RIPOTI YA MAPATO NA MATUMIZI


Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umetoa ripoti ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miezi sita tangu Januari 14, 2013 mpaka Julai 14, 2013 ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutoa mahesabu hayo kwa wapenzi, washabiki, na wanachama na jamii  kwa ujumla.
Baadhi ya gharama kubwa kwa klabu ni pamoja na usajili wachezaji na mishahara.Akiongea na waandishi wa habari juu ya mahesabu hayo katibu mkuu wa Young Africans Lawrence Mwalusako amesema mapato makubwa ya klabu yanatokana na viingilio vya mechi na ufadhili.
  • Juhudi mbalilmbali zinafanyika kuongeza kipato cha klabu kama kuingia mikataba ya ufadhili, kutumia haki miliki za klabu.
  • Uongozi unajitahid kuweza kudhibiti matumizi ya klabu kama njia moja ya kuhakikisha klabu inajitegemea.
  • Klabu bado inaendelea kutegemea ufadhili wa TBL ambao kwa sasa inapata wastani wa mIL 30.25 kila mwezi, Madhumuni ya ufadhili huu ni kuwezesha klabu kulipia mishahara ambayo wastani inzaidi mil 60 kwa mwezi. Tayari klabu imeshaomba mazungumzo na mfadhili kuboresha mkataba huo.
  • Katika kipindi cha Januari 2013 hadi Julai 2013 klabu iliweza kupata mil 110 kama zwadi mbalii mbali za ushindi ikiwemo mil 15 kutoka vodacom kwa kuwa timu yenye nidhamu.
  •  Bado kuna mali za klabu hazija thaminiwa zikiwemo majengo
 

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger