BALLON D'OR: KOCHA WA UJERUMANI AGOMA KUPIGA KURA ZA KUMCHAGUA MWANASOKA BORA WA DUNIA

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amekataa kupiga kura katika mchakato wa kumchagua mwanasoka bora wa dunia mwaka huu, shirikisho la soka la Ujerumani limethibitisha. 

Wachezaji wake watano wapo katika kinyang'anyiro hicho: Mastaa wa Bayern Munich Manuel Neuer, Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller, na kiungo wa Arsenal Mesut Ozil.

Lakini kwa sababu kura zote binafsi huwekwa hadharani baada ya sherehe za tuzo, boss wa Mannschaft ameamua kuepeukana na kusababisha hali ya kuonekana ana upendeleo kwa mchezaji fulani kwa kupiga kura hiyo ya Ballon d'Or.

"Ameshindwa kupiga kura kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wake na hivyo ameonelewa kuepukana na zoezi hilo," msemaji wa DFB  Jens Gritter aliiambia Sport Bild.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger