Wyclef Jean awasili Lagos nigeria tayari kuwa MC show ambayo Vanessa Mdee atatumbuiza pamoja na wakali wengine wa Nigeria

Vanessa Mdee aka Vee Monoey ndiye msanii pekee wa Tanzania ambaye amepata nafasi ya kutumbuiza katika show kubwa nchini Nigeria ya ‘Rythm Unplugged 2013’ ambayo inatarajiwa kufanyika kesho na host wa show hiyo atakuwa msanii wa Marekani Wyclef Jean.
Wyclef Jean in nigeria Wyclef baada ya kuwasili Naija
Wyclef Jean tayari amewasili nchini humo kwa ajili ya show hiyo kubwa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka, na kuhusisha wasanii wakubwa wa Naija wakiwemo P-Square, Wiz Kid, Davido, D’Banj na wengine.
Wyclef Jean in lagos
Jean alitweet masaa machache kabla hajaondoka Marekani, “I am on my way to Africa today !v “Nigeria” “Ghana” We all Love Nelson Mandela! Then I will be in Jamaica my second home performing at “sting”.
Hii ni mara ya pili kwa Wyclef kwenda Nigeria kuhost tamasha la muziki, baada ya ile ya MTV Africa Music Awards.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger