FAMILIA YA MAREHEMU DKT MVUNGI YAWASAMEHE WALIOMUUA..! SOMA ZAIDI HAPA



Familia ya marehemu Dk Edmund Sengondo Mvungi pamoja na chama cha NCCR-Mageuzi kimewasamehe wale wote waliohusika na kumuua Dkt Mvungi ambaye alikuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba

Rai hiyo imetolewa na msemaji wa familia ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James francis Mbatia wakati wa ibaada maalum ya kumwombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam

Mbatia amesema Tangu marehemu Dkt Mvungi alipopata tazito la kuvamiwa na watu waliomkata mapanga Novemba 3 mwaka huu hadi mauti yalipompata Novemba 12, yamesemwa maneno mengi, lakini wao kama familia na chama wameamua kuwasamehe wauaji wote

"Tunasema kwamba tumewasamehe, damu ya Dkt Mvungi imeshamwagika, alikuwa mpigania nchiniwe na katiba mpya, sasa amekufa lakini tunafurahi kuona mchakato wa katiba mpya unaendelea na ndiyo ilikuwa dhamira yake"alisema Mbatia

Dkt Mvungi alivamiwa na kukatwa mapanga nyumbani kwake Kibamba jijini dar es salaam hali iliyopelekea kifo chake wakati akipatiwa matibabu nchini Afrika kusini novemba 12 mwaka huu.
Credit:edwinmoshi.com

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger