AZAM YASIMAMISHA USAJILI KUMSUBIRI KOCHA MPYA MCAMEROON




 
OMONG
Uongozi wa Azam umekubaliana kwa pamoja kusitisha mipango yote ya usajili mpaka kocha wao mpya, Joseph Omog, raia wa Cameroon, atakapofika.

Taarifa ambazo Championi Jumatano limezipata kutoka ndani ya Azam FC, zimesema uongozi wa timu hiyo umeona usitishe zoezi la kusajili au kuwaacha nyota  wa timu hiyo, mpaka kocha wao huyo atakapowasili na kuiona timu.
Bosi mmoja (jina tunalo), amesema tayari timu hiyo ilikuwa na majina ya nyota waliotakiwa kusajiliwa katika kikosi hicho pamoja na wale wanaoachwa. Kufuatia mapendekezo aliyoyafanya awali aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Muingereza, Stewart Hall, kazi hiyo imesitishwa mpaka kocha mpya atakapoleta tathmini yake.
“Asikwambie mtu kwamba tunasajili mchezaji yeyote kwa sasa, Azam kama unavyoona tupo kimya tukisubiri kwanza kocha wetu mpya afike ili atupe kile anachokiona katika timu, aongezewe kipi na kipi kiondolewe,” alisema bosi huyo na kuongeza:
“Uongozi wetu hautaki kumsajilia kocha wachezaji, mpaka sasa tulikuwa na mapendekezo mbalimbali aliyoyafanya Stewart kabla ya kutangaza kuondoka, lakini hakuna kitakachofanyika katika hilo,” kilisema chanzo hicho.
 SOURCE: CHAMPIONI

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger