HULK, ROBINHO WAIZAMISHA CHILE 2-1 HUKO TORONTO, NEYMAR AIBUKA NYOTA WA MCHEZO
Wednesday, 20 November 2013 08:21
>>NEYMAR HAKUFUNGA LAKINI NYOTA WA MCHEZO!!
WAFALME wa Soka Duniani, Brazil, ambao pia ndio Wenyeji wa Kombe la Dunia Mwaka 2014, Alfajiri hii huko Rogers Centre, Toronto, Canada waliitandika Chile Bao 2-1 katika Mechi ya Kirafiki.
Neymar, ambae hakufunga, ndie alikuwa
Nyota wa mchezo wakati Brazil ikiendeleza wimbi la kutofungwa katika
Mechi 12 na Chile linaloanzia Agosti Mwaka 2000.
Robinho ndie alieifungia Brazil Bao la
ushindi katika Dakika ya 79 baada ya Chile kusawazisha Bao la kwanza
lililofungwa na Hulk huku Mfungaji wa Chile akiwa Eduardo Vargas.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Brazil 2
-Hulk Dakika ya 14
-Robinho 79
Chile 1
-Eduardo Vargas Dakika ya 71
+++++++++++++++++
Ijumaa iliyopita Chile ilikuwa Mjini
London Uwanja wa Wembley ambapo waliifunga England Bao 2-0 na Brazil
kuwa huko Miami, USA ambako waliichapa Honduras Bao 5-0.
VIKOSI:
BRAZIL: Júlio César,
Maxwell, Maicon, Thiago Silva [Dante], David Luiz, Luiz Gustavo,
Paulinho [Hernanes], Oscar [Willian], Jô [Robinho], Hulk [Ramires],
Neymar [Lucas Leiva]
CHILE: C. Bravo, M.
González, G. Jara, E. Mena, M. Diaz [J. Beausejour], J. Fuenzalida [J.
Valdivia,=M. Fernández], G. Medel, C. Carmona, F. Gutiérrez [C. Muñoz],
A. Sánchez, E. Vargas
Refa: S. Petrescu