Kiwango cha Mesut Ozil dhidi ya Southampton kilikuwa bora kuliko kiwango alichokionyesha katika mechi za hivi karibuni.

Kiungo huyo mwenye thamani ya £42.5 million alihusika sana na mchezo siku hiyo. Alicheza vizuri na washambuliaji wenzie katika kutengeneza mashambulizi yaliyoiwezesha Gunners kutoka na ushind dhidi ya timu ngumu ya Southmpton. 
Kiwango kizuri cha Ozi inawezekana kabisa kimetokana na kupata mapumziko wakati wa wiki ya michezo ya kimataifa. Kuumwa na kucheza mechi nyingi bila kupumzika kumemfanya apunguze kasi tangu alipojiunga na Arsenal akitokea Real Madrid.
Clive Rose/Getty Images
Pamoja na kiwango chake kuimarika, kuna hisia kwamba Ozil bado hajafikia kwenye fomu aliyokuwa nayo Madrid wakati alipojitambulisha kwenye ulimwengu kama mmoja wa viungo bora wa kushambulia duniani. 
Ni kweli Ozil amekuwa na mchango chanya katika timu, lakini bado hajaonyesha haswa kilichoifanya Arsenal kuvunja rekodi ya usajili. Aaron Ramsey na  Santi Cazorla kiasi kikubwa wamefunika nyota yake. 
Kiukweli na uhalisi zaidi, Ozil amekuwa na mchango mkubwa wa kiakili zaidi kuliko uwanjani.
Wakati alipowasili, alibadili mambo ndani ya Arsenal. Kusajiliwa kwa Ozil ilikuwa ni kama taarifa ya Arsenal kwa dunia kwamba bado ni timu kubwa yenye uwezo wa uvutia wachezaji bora - hii ni taarifa iliyosikika vizuri kwa wachezaji na mashabiki pia.
Wachezaji wa Arsenal walifahamu klabu inahitaji kusaini japo mchezaji mmoja mwenye jina ili kukiongezea nguvu chao ambacho kilikuwa kinakosa ubora wa kushindani ubingwa. Ozil amecheza sehemu kubwa katika kuirudisha hali ya kupambana ya wachezaji wa Arsenal. Mchango wake mkubwa kwa Arsenal umekuwa nje ya uwanja. 
Ni kweli, yeye ni mmoja ya wachezaji wawili wenye assists nyingi katika premier league pamoja na kutocheza michezo kadhaa ya mwanzo mwa ligi, lakini hakuna anayeweza kubisha kwamba Ozil., ambaye aliweza kuwa mmoja wa viungo wa washambuliaji bora kabisa dunia akiwa na Real Madrid, bado hajaonyesha uwezo wake wote pale Emirates.
Lakini inabidi ukumbuke, hata gwiji wa soka wa klabu hiyo Robert Pires alichukua muda mrefu kuweza kuimudu ligi kuu ya England ambayo inatumia nguuvu zaidi. 
Mjerumani huyu pia amekuwa akisumbuliwa na majeruhi pamoja na uchovu kutokana na kucheza mechi nyingi, hivyo kuna sababu kadhaa zinazomfanya bado asifikie ubora wake. 
Kwa bahati nzuri kwa Arsenal, wachezaji waliokuwepo kabla ya Ozil wamezidi kuwa bora na kuimarika kiuchezaji na ndio maana timu haijaathirika kutokana kukosa huduma nzuri kwa Ozil. 
Lakini Ozil ametengeneza imani ndani ya kikosi kwamba Gunners ni timu kubwa na yenye uwezo wa ksuhinda makombe. Uwepo wake unaipa timu nzima moyo wa kujituma kwa sababu kila mchezaji anajua Ozil anaweza kubadilisha matokeo muda wowote. 

Ukweli wa kwamba Ozil bado hajafikia uwezo wake wa juu usije ukakuzuia au kudharau mchango wake mkubwa aliotoa Arsenal. Akiwa bado hajakaa sawa lakini tayari ameonyesha kuongoza mapinduzi ndani ya klabu hiyo. Fikiria Arsenal ingekuwa wapi kama Ozil angekuwa kwenye kiwango .
source: shafii dauda