Wachezaji wake watano wapo katika kinyang'anyiro hicho: Mastaa wa Bayern Munich Manuel Neuer, Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller, na kiungo wa Arsenal Mesut Ozil.
Lakini kwa sababu kura zote binafsi huwekwa hadharani baada ya sherehe za tuzo, boss wa Mannschaft ameamua kuepeukana na kusababisha hali ya kuonekana ana upendeleo kwa mchezaji fulani kwa kupiga kura hiyo ya Ballon d'Or.
"Ameshindwa kupiga kura kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wake na hivyo ameonelewa kuepukana na zoezi hilo," msemaji wa DFB Jens Gritter aliiambia Sport Bild.