COASTAL BINGWA UHAI 2013, YANGA WACHAPWA 2-0 KAMA WAMESIMAMA

4_e8d82.jpg
Na Princess Asia, Dar es Salaam
COASTAL Union ya Tanga imetwaa ubingwa wa michuano ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, kwa klabu za Ligi Kuu ya Bara maarufu kama Kombe la Uhai, baada ya kuifunga Yanga SC ya Dar es Salaam mabao 2-0 jioni hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua, Coastal ilipata mabao yake kupitia kwa Ally Nassor dakika ya 52 na Mahadhi Juma dakika ya 89.
Ushindi wa leo wa Coastal ni sawa na kulipa kisasi cha kufungwa 2-1 na Yanga katika mechi ya kundi lao hatua za awali za mashindano hayo Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Kwa kutwaa ubingwa huo, Coastal wamezawadiwa Sh. Milioni 2 na wadhamini wa michuano hiyo, maji bora ya Uhai wakati washindi wa pili Yanga wamezawadiwa Sh. Milioni 1.5 na Azam FC walioshika nafasi ya tatu wamepewa Sh. Milioni.
Mtoto wa beki wa zamani wa kimataifa Tanzania, Salum Kabunda 'Ninja Msudan' (sasa marehemu) aitwaye Ally Salum Kabunda wa Ashanti United ameibuka mfungaji bora wa mashindano kwa mabao yake tisa, ingawa timu yake iliishia Robo Fainali na kutolewa na Yanga

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger