Msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa umeingia Kigoma tayari, ukianzia Wilaya ya Kakonko.
Hivi sasa ni mkutano wa kwanza Kijiji cha Muhange, Kata ya Muhange. Amepata mapokezi mazuri sana huku akina mama, watoto, vijana na wazee wako mkutanoni.
Mkutano wa pili utakuwa jioni Kakonko mjini.
Source:Afisa Mwandamizi Habari CHADEMA Tumaini Makene