HUYU NDIO MCHEZAJI WA MPIRA WA MIGUU BORA AFRIKA KWA MUJIBU WA TUZO ZA BBC
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, aliwashinda wachezaji wenzake Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa na kuibuka mshindi wa tuzo hiyo.
Yaya toure ndani ya miaka minne mfululizo ameingia kwenye kinyang’anyiro hiko.
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu,Hatimae kile kinyang’anyiro cha mwanasoka bora wa Bbc kimemalizika,Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika ya BBC kwa mwaka 2013.