|
Mhe. Angela Kairuki akitembelea Jeshi la Magereza katika mojawapo ya shughuli zake za kikazi Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Angela Jasmine Kairuki (37) ametajwa katika jarida la kimataifa la Forbes kuwa ni mmoja wanawake vijana 20 wenye nguvu barani Afrika mwaka huu. Katika toleo lake la hivi karibuni chini ya kichwa cha habari 'The 20 Young Power Women in Africa 2013', jarida la Forbes linamuorodhesha Mhe Kairuki sambamba na wanawake wengine 19 kama vijana wa kike wenye nguvu kwa nafasi zao kikazi na kibiashara.(P.T)
Kutajwa kwa Mhe Kairuki katika orodha
hiyo kumezua msisimko katika mawasiliano ya mtandao wa 'twitter' ambapo
Watanzania wengi wamekuwa wakielezea furaha na fahari zao kwa kuona
Mtanzania mwenzao, tena mwanamke kijana, anatambulika kimataifa kwa
utendaji wake.
|
Wengine ni Rapelang Rabana (Afrika Kusini) Mjasiriamali, Claire Akamanzi (Rwanda) Afisa Mtendaji Mkuu wa Rwanda Development Board, Valentina da Luz Guebuza (Msumbiji) Mwekezaji, Hadeel Ibrahim (Sudan) wa Mo Ibrahim Foundation, Alengot Oromait (Uganda) Mbunge, na Monica Musonda, (Zambia) Afisa Mtendaji Mkuu na MWanzilishi wa kampuni ya Java Foods.
Wengine ni NoViolet Bulawayo (Zimbabwe) Mtunzi wa vitabu, Minoush Abdel-Meguid (Misri) Mwekezaji, mjasiriamali na mwendesha benki, Ola Orekunrin (Nigeria) Daktari na Mwanzilishi wa The Flying Doctors, Sibongile Sambo (Afrika Kusini) Afisa Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi wa SRS Aviation, Lupita Nyong’o (Kenya) Mwigizaji na mtengeneza filamu, Amini Kajunju (Congo DRC) Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Africa-America Institute na Folake Folarin-Coker (Nigeria) Mbunifu wa mitindo.
Wengine katika orodha hiyoni Lindiwe Mazibuko (Afrika Kusini) Mwanasia na Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance (DA) bungeni, Minoush Abdel-Meguid (Misri) Mwekezaji, Mjasiriamali na mwendesha benki, Sibongile Sambo (Afrika Kusini), Wangechi Mutu, (Kenya) Msanii na mchongaji.