Ukiachana na mitindo yake ya kunyoa nywele (kiduku), huku kichwani kukiwa na urembo wa maandishi kama wafanyavyo wasanii au wachezaji wa mpira, Seneta huyo huwa ni mtu wa kupiga pamba na bling bling shingoni, masikioni na vidole vyake huchafuliwa na gold, kuna uwezekano akisimama na Octopizzo unaweza ukahisi Sonko ndiye msanii na Octo ni dereva wake. (Joke)
Mtandao wa Nairobi Wire umeweka picha ya simu ya mezani inayotumika katika ofisi ya Seneta huyo wa Nairobi, yenye mfano wa umbo la msichana aliyevaa bikini pamoja na bra zenye bendera ya Uingereza. Katika picha hiyo Sonko anaonekana akiongea
kupitia simu hiyo.
PICHA: NAIROBI WIRE