Ingawa Yanga ina mastraika wengi lakini upo uwezekano mkubwa wa kuongeza straika mwingine wa maana kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika na hata kwa ajili ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.
Mastraika waliopo kwa kiasi kikubwa wameonekana bado hawana kiwango ambacho Kocha Mkuu, Ernest Brandts anakitaka.
Brandts kila mara amekuwa akilalamikia washambuliaji wake kutokuwa makini na kukosa mabao ya wazi na aliwahi kupendekeza atafutwe straika mmoja wa maana hasa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.
Yanga ina mastraika sita ambao ni Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerry Tegete, Shaaban Kondo, Said Bahanuzi na Hussein Javu.(P.T)
Kati ya hao Kiiza, Kavumbagu na Tegete
ndio wamekuwa wakipata nafasi ya kucheza mara kwa mara wakati wengine
waliobaki wamekuwa wakisugua benchi na wengine kugeuka watazamaji
jukwaani.
Kiiza ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao ndani ya timu hiyo, amefunga mabao manane akifuatiwa na Kavumbagu na Tegete waliofunga mabao matano kila mmoja.
Brandts aliliambia Mwanaspoti kuwa kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa upande wa washambuliaji na hilo ndio analolipa mkazo katika usajili wa nafasi iliyobaki.
"Washambuliaji ninao wengi lakini bado hawajaweza kucheza na kufunga mabao katika kiwango ninachotaka hivyo katika eneo hilo nahitaji kuongeza nguvu hasa kwa ajili ya mashindano makubwa ya kimataifa," alisema Brandts.
Kikosi cha Yanga kina wachezaji 27 mmoja akiwa ni Omega Seme anayecheza kwa mkopo Prisons ya Mbeya na kwa mujibu wa TFF, timu haipaswi kusajili kwa pengo la mchezaji aliyepelekwa kwa mkopo.
Kwa maana hiyo,Yanga katika usajili huu mdogo ina nafasi ya kusajili wachezaji watatu tu, na tayari imeshawasajili wawili; kipa Juma Kaseja na kiungo Hassan Dilunga hivyo wamebakiwa na nafasi moja.
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto aliliambia Mwanaspoti kwamba, wana nafasi moja tu ya kusajili ambayo hata hivyo uongozi bado unapambana kuhakikisha wanasajili mchezaji atakayeisaidia timu.
Mwanaspoti linafahamu, Yanga inahitaji kusajili straika wa maana na kama ikishindikana apatikane beki anayemudu kucheza nafasi zaidi ya moja.
Yanga inadaiwa kuwa katika mazungumzo na beki wa kushoto wa Coastal, Abdi Banda wa Coastal Union japokuwa bado wanaumiza vichwa kuhusu nani asajiliwe kati ya beki na straika.
"Muda wa usajili bado unaendelea na mambo yanafanywa na viongozi, muda ukifika tutaweka wazi kila kitu, lakini jambo la muhimu ni kwamba tuna nafasi moja ya kusajili," alisema.
Alipoulizwa Kocha wa Yanga, Ernest Brandts alisema anafahamu ana nafasi moja tu ya kusajili hivyo anashirikiana na viongozi kujua wanamsajili mcheza yupi na kwa manufaa yapi.
Mabeki wa kushoto waliopo Yanga ni David Luhende na Oscar Joshua ingawa siku za karibuni Luhende amekuwa majeruhi wakati Joshua hakubaliki sana na kocha.