TAARIFA YA CHADEMA MKOA WA ARUSHA BAADA YA OFISI ZAO KUCHOMWA MOTO
Matukio yanayokiandama chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] yamezidi kuchukua nafasi ambapo mkoani Arusha watu wasiojulikana wameshutumiwa kuchoma moto ofisi za chama hicho Jumanne tar 03 Dec 2013 asubuhi na kusababisha uharibifu mdogo.
Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Mchungaji Amani Golugwa amesema ‘Mpaka hivi sasa tunavyoongea eneo la ofisi ndani ya ofisi kabisa eneo la bafu na choo limeungua na upande wa juu wa bati umeungua na kikubwa zaidi walitaka kuingia chumba cha computer room ambacho tunahifadhi data kwa wanachama wetu kwa kanda nzima ya kaskazini majimbo 33 sasa hivi’
‘Sasa baada ya kushindwa hiyo ndo wakatengeneza shoti ya umeme pakashika moto, tunamshukuru Mungu tu kwamba huu moto haukuendelea sana kwa hiyo athari haipo kwenye nyaraka zozote wala kwenye machine zilizopo hapa ofisini’ – Golugwa