TAKUKURU KWA KUSHIRIKIANA WADAU WA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA WAANDAA TAMASHA JIJINI ARUSHA



DSC_0043
Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya ushauri wa Umoja wa Afrika ya kupambana na Rushwa yaani African Union Advisory Board on Corruption (AUABC) na Tamasha la wasanii lenye lengo la kufikisha ujumbe juu ya Madhara ya Rushwa kwenye Jamii, Kati kati ni Emmanuel Atenga toka (AUABC) na Stephane Ndilimbaye toka AUABC.
--
Na.Mwandishi wetu
TAASISI YA KUPAMBANA NA KUZUIA RUSHWA (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) na Megamark Ltd wameandaa tamasha kubwa litakalowashirikisha wasanii mbali mbali toka Tanzania, Kenya na Uganda katika kuadhimisha miaka 10 tangu bodi hiyo ya Afrika katika maswala ya Rushwa kuanzishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark ltd, Chedi Ngulu amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kufikisha ujumbe kwa umma juu ya kupambana na Rushwa na kuelezea madhara ya Rushwa kwenye jamii na nchi kwa ujumla.
DSC_0063DSC_0075
Bw. Emmanuel Atenga (wa pili kushoto) kutoka na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo litakalofanyika tarehe 7 mwezi ujao katika viwanja vya General Tyre Arusha. Kulia ni mmoja wa wasanii wataoimba kwenye Tamasha hilo Fid Q na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu na kushoto ni Stephane Ndilimbaye kutoka AUABC.

“Muziki upo katika asili ya waafrika na umekuwa ukitumika kuburudisha lakini zaidi kufikisha ujumbe wenye kujenga na kurekebisha jamii (Hadhira) iwe ni nyimbo, kughani ambayo tunatambua kwa njia ya Rap na ngoma za asili, lakini tumechagua muziki kama njia rahisi ya kufikisha ujumbe hasa kwa vijana kuhusu madhara ya Rushwa,” amesema Ngulu.

Amesema kuwa katika tamasha hilo nyimbo mbalimbali zitaimbwa katika kuelezea matatizo ya Rushwa kwenye jamii na hasa kuelimisha vijana umuhimu wa kukataa Rushwa kwa sababu vijana ndio nguvu kazi ya taifa na asilimia 75 ya watu nchini ni vijana.

“kwa mantiki hii, tumeandaa onyesho lenye anuani isemayo “Rushwa sio” ikimaanisha rushwa haina manufaa na ni yenye kutakiwa kupigwa vita kwa gharama yoyote ile,”
DSC_0095
Msanii Fid Q akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo.
“Onyesho hili litafanyika Arusha tarehe 7 mwezi wa kumi na mbili katika viwanja vya General Tyre kuanzia saa saba na nusu mpaka saa kumi na mbili jioni na litahusisha wasanii wenye kukubalika na jamii,” alisisitiza

Kwa upande wake, Emmanuel Atenga toka Kitengo cha Mawasiliano (AUABC) amesema Board hiyo ya Umoja wa Afrika ya kupambana na rushwa imepata mafanikio kwa kuanzisha vitengo vya ufatiliaji kwa wanachama wa Umoja wa Afrika wenye lengo la kusaidiana katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Amesema mapambano dhidi ya rushwa Afrika yanahitaji nguvu ya pamoja kwa ksuhirikisha jamii wakiwemo wasanii katika kuhamasisha mapambano ya kukataa Rushwa kwenye ngazi zote ndani ya nchi na bara zima la Afrika.
DSC_0036
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
DSC_0039
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger