hatimaye okwi atua yanga rasmi,

Emmanuel Okwi.
Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Emmanuel Okwi kutoka klabu ya SC Villa.
Yanga wamelipa kiasi cha dola za Kimarekani 20,000 kama ada ya uhamisho na kumsainisha Okwi mkataba wa miaka miwili.
Okwi anatarajia kuwasili nchini hivi karibu akitokea Uganda, ameiomba Yanga abaki nchini Uganda kumalizia kufanya tangazo la kampuni moja ya simu nchini humo.
Hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC ) imepatikana leo saa tisa mchana.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger