CHIDI BENZ AMEVURUGWA KWELI..!! TAZAMA ALICHOKIONGEA KATIKA POST YAKE



Hakuna tena kitu kizuri kwa Chidi Benz siku hizi. Kwa muda mrefu rapper huyo ambaye hivi karibuni ametokea kukubalika sana nchini Kenya (thanks kwa mashavu anayopewa na Nonini) ameonekana kutoa yake ya rohoni yanayomuumiza kupitia Twitter.

Yeye na Wakazi kuna tatizo?
Picha lilianza jana, baada ya Wakazi kutweet: Na ningependa kusema pia AY, Dimpoz, Ally Kiba, FidQ, Shaa, Cpwaa, Black Rhino, Remi Ongala, Profesa Jay & Lady Jaydee ni other Local heros!
Baada ya kuona ujumbe huo wa Wakazi, Chidi alimuuliza kishari ‘nini?’
Wakazi alichuna. Chidi akaamua kuandika: Hujui kuongea huwezi muoga..unaweza kuandika hapa twitter. Nyie ndio mkianza kushindwa mnasifia maadui.#umal** tuu.”
Ujumbe huo ulivuta hisia za watu wengi akiwemo Madee aliyeuliza: Rasheeed nani tena kazingua?  Chidi alijibu:Mazafanta wanahisi wanajua kuliko wewe wakati mwenyewe saa zingine unaona hujijui..2
Hata hivyo hatuwezi kuthibitisha kama maneno hayo yalikuwa yakimlenga Wakazi ama mtu mwingine kwakuwa kabla ya hapo tayari alikuwa ameanza kuandika tweets za hasira.
“Game ilipo now na propaganda zake inaua vitu vingi tu.sisi tunaonekana tunalalamika ujinga but hatuna maisha mabaya. Viongozi wa nchi sio lazima mdil na bongo freva..haiongezi wewe kufatwa but unatuongezea uadui usio na lazima. Mi natangazwa kwa ubaya tuuuuu.ila nina marafiki bado na wengi wanaongezeka hata hapa.#nakaza roho,” aliandika Chidi.
Kunani?

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger