NINI SABABU YA PENNY KUKONDA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI



Stori: Imelda Mtema
MTANGAZAJI wa Runinga ya DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameamua kujikondesha mwili ambapo amefanikiwa kupoteze uzito usiopungua kilo 18 mwilini.

Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Penny alifunguka kuwa, kutokana na kuona mwili wake unavimbiana, aliamua kufanya mazoezi maalum ya kupunguza mwili sambamba na kufanya ‘dayati’ ambayo imembadilisha muonekano wake (tazama picha ndogo).
“Nimeamua tu kuubadilisha muonekano wangu wa unene kwani nilikuwa ninazidi kuwa bonge, kweli nimefanikiwa maana hata uzito nimepungua kwa sasa.
“Kabla sijaanza kufanya mazoezi nilikuwa na kilo 85 lakini sasa nimepungua hadi kufikia kilo 67, ni mafanikio makubwa ambayo nimeyapata katika zoezi langu la kupunguza uzito,” alisema Penny ambaye ni ‘ubavu’ wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Kuhusu msosi, kwa sasa Penny asubuhi anakula ‘ma-apple’ mawili au kipande cha papai, mchana anakunywa juisi na usiku anamalizia na saladi ya samaki au kuku, analala.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger