Mtibwa walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 14, mfungaji Shiza Kichuya na Yanga wakasawazisha kupitia kwa Notikel Masasi dakika ya 17 ambaye pia alifunga la pili dakika ya 32 kabla ya na Hamisi Issa kufunga la tatu dakika ya 86.
Yanga sasa itamenyana na Coastal Union iliyowatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Azam FC jana kwa kuwafunga 1-0 katika fainali Jumapili kwenye Uwanja huo huo wa Azam Complex.
Katika hatua ya makundi, Yanga iliifunga 2-1 Coastal Union, je fainali mambo yatakuwaje?(P.T)