MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA TAIFA HUDUMA ZA FEDHA NCHINI.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ,
Prof. Benno Ndulu, akisaini mfano wa cheti cha Mpango wa Taifa wa
Huduma za Fedha wenye lengo la kusimamia na kutafuta ufumbuzi wa
changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Wanaoshuhudia nyuma
(katikati) ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, kulia kwake ni Malkia Maxima wa Uholanzi
(kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha Sada Mkuya Salumu. Hafla hiyo
imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania,
jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha, wenye lengo la Kusimamia
na kutatua ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za fedha
nchini. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu
ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Malkia Maxima wa Uholanzi, akihutubia
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye
lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa Changamoto zinazozorotesha
huduma za fedha nchini. Hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Mohammed Gharib Bilal imefanyika leo kwenye
ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, leo.
Picha na OMR
Malikia Maxima wa Uholanzi, akibofya
kitufe kama ishara ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha.
Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR(P.T)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Malkia Maxima wa
Uholanzi na Naibu Waziri wa Fedha, Sada Mkuya Salumu, wakiwa
wameshikilia Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha baada ya kuzinduliwa leo
kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania. Picha na OMR
Baadhi ya wadau wa Sekta za Fedha
waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal,
alipokuwa akihutubia, wakati wa uzinduzi.