BABY MADAHA AKOLEA KIMAHABA NA MENEJA WAKE


 STAA wa filamu Bongo anayetamba na ngoma yake ya Summer Holiday amesema kuwa kutokana na mahaba mazito anayopatiwa na mwandani wake Joe Kariuki ambaye ni Meneja wake hafikirii kumuacha kamwe.
 
Akistorika na paparazi wetu alisema, tangu aanze uhusiano na pedeshee huyo anayemiliki studio ya Candy n’ Candy  nchini Kenya, amekuwa akijiona mwenye fahari kubwa kwenye sayari ya mapenzi kutokana na upendo anaomuonesha na kumfanya asiwaze kumpotezea kamwe.
“Kusema kweli huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi lakini abadani sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na uhusiano naye ila porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo natamani niamie Kenya ili tuwe karibu wakati wote,”alisema Baby Madaha.
Aliongeza kuwa kikubwa kilichompelekea kuwa naye ni kutokana na upendo wake wa kweli alionao kwake siyo kutokana na suala la mkwanja kama wengi wanavyodhani.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger