Gari lenye namba za usajili T 704 ADR aina ya Scania bus la kampuni ya CHAMPION.
Gari
lenye namba za usajili T 704 ADR aina ya Scania bus la kampuni ya
CHAMPION likiendeshwa na dereva ALLY RAMADHANI, mnyaturu, umri kati ya
35 - 40, mkazi wa Kisasa Dodoma likiwa limebeba wanamichezo/wanavyuo wa
vyuo vikuu vya Zanzibar na State University Zanzibar likitokea chuo
kikuu Dodoma (UDOM) likielekea kituo kikuu cha mabasi Dodoma lilipinduka
na kusababisha majeraha kwa abiria wapatao 43 kati yao Majeruhi 29
waliotibiwa na kuruhusiwa na majeruhi 14 wamelazwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa Dodoma, wote wakiwa ni wanaume.
Akiongea
na waandishi wa habari ofisini kwake Kamishna msaidizi wa Polisi SUZAN
S. KAGANDA amesema ajali hiyo imetokea tarehe 15/12/2013 majira ya saa
06:15 hrs huko eneo la mlima wa Chimwaga UDOM Kata ya Makulu
Dodoma mjini.
Kamanda KAGANDA amewataja majeruhi katika ajali hiyo ambao ni:-
1. Hamisi Hamisi, miaka 28, mshirazi, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
2. Bashiru Yusuph, miaka 26, sukuma, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 1.
3. Abdallah Juma, miaka 28, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word namba 1.
4. Ally Sharifu, miaka 24, mshirazi, mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
5. Mussa Mkanga, miaka 21, mzanzibari, Mwanachuo. Amelazwa word namba 1.
6. Seifu Fakii juma, miaka 27, mshirazi, mwanachuo State University. Amelazwa word 1
7. Ahamed Mohamed Hassani, miaka 23, Mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University. Amelazwa word namba 11.
8. Richard Mwasonga, miaka 36, mnyiha, Tingo wa bus, Miyuji Dodoma. Amelazwa word namba 1.
9. Juma Nasoro, miaka 23, mshirazi, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.
10. Hemedi Mohamed, miaka 29, Mzanzibari, mwanachuo State University Zanzibar. Amelazwa word namba 1.
11. Mussa Mtaugana, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University
12. Adam Mwale Bonifasi, miaka 24, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University.
13. Amelazwa word namba 1.
14. Mohamed Ally Mohamed, miaka 23, mzanzibari, mwanachuo Zanzibar University.
15.
Nassoro Mohamed Saidi, miaka 25 -30, mwanachuo
State University Zanzibar. Hali yake si nzuri sana na amelazwa chumba
cha wagonjwa mahututi (ICU).
Aidha
Kamanda KAGANDA amesema Chanzo cha ajali ni mteremko mkali wenye kona
iliyosababisha dereva kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha ajali
ya gari kupinduka upande wa kulia na kulala kiubavu. Mara baada ya ajali
hiyo dereva alikimbia kwenda kusikojulikana na juhudi za kusaka dereva
huyo zinaendelea. Pia uchunguzi unaendelea kubaini iwapo gari hilo
lilikuwa na tatizo lolote.
Jeshi
la Polisi mkoa wa Dodoma linatoa Wito kwa madereva kila mara wawe
makini barabarani hasa kipindi hiki cha mvua na kuwa makini hususani kwa
barabara zenye milima.