KAMA WEWE BADO HUJAJIUNGA NASI, UNAWEZA KUJIUNGA HAPA MOJA KWA MOJA ONLINE <<<BOFYA HAPA NA LIKE PAGE YETU>> : |
Baadhi
ya wasanii chipukizi kutoka anga ya muziki wa Bongofleva pia walipewa
nafasi ya kuonesha umahiri wao wa kulishambulia jukwaa vilivyo.
Watangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu na Dj Fetty wakijadiliana jambo nyuma ya jukwaa.
Mashabiki wakifurahi burudani iliyokuwa ikitolewa juu ya steji
DJ
Mahiri kutoka Clouds FM akifanya makamuzi ya nguvu ndani ya Mbalamwezi
Beach,wakati wa tamasha la After Skull Bash likiendelea,Tamasha hilo
limewakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali.
Msanii
Nguli wa muziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda a.k.a Mtoto wa Mama Said
akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la After
Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini
Dar.
Mmoja
wa watangazaji mahiri wa Clouds FM,Hamis Mandi a.k.a B Dozen akitoa
utaratibu mzima wa tamasha hilo utakavyofanyika.Tamasha hilo
limeratibiwa na Clouds FM kwa kushirikiana na kampuni bingwa ya burudani
hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd.
Msanii
wa muziki wa Kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga ya
muziki wa bongofleva,Rich Mavoko akikamua vilivyo jioni ya leo kwenye
tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa
Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.
Mashabiki waliofika kwenye tamasha hilo wakifuatilia kwa makini.