KIJANA aliyefahamika kwa jina la Abdul
Kiba amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukamatwa akiwa na simu
inayodaiwa kuwa ni ya wizi na ‘kuswekwa’ sero kufuatia jitihada za ndugu
zake kumuwekea mdhamana kugonga mwamba, Ijumaa limetonywa.
Tukio hilo lilijiri Jumanne ya wiki hii katika viwanja vya Karume jijini Dar, wakati kijana huyo alipokuwa akicheza mpira.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichokuwa uwanjani hapo, muda mfupi baada ya mchezo huo kumalizika, ndipo Abdu akawekwa chini ya ulinzi wa polisi wa kituo cha Msimbazi, kwa tuhuma ya kuwa na simu ya wizi aina ya Samsung Galaxy yenye thamani ya shilingi laki nane, ambayo inadaiwa kuwa mali ya mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Abdallah Muhidini.

Katika mahojiano yake na Polisi, Abdul
alijitetea kuwa simu hiyo aliuziwa na vijana wawili siku za hivi
karibuni aliowataja kwa majina ya Shaaban Rajab au Kibabu kama
anavyojulikana kwa wengi (anayeshikiliwa na polisi).
Hata hivyo licha ya utetezi huo, Abdul alifunguliwa kesi jalada Na. MS/RB/12267/2013 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia
ya simu, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Juma
Bwire alithibitisha kukamatwa Abdul Kiba na kwamba upelelezi bado
unaendelea.