STAA wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amenusurika kubakwa na vijana wa kihuni nchini Kenya maarufu kama machokoraa.
Tukio hilo lilitokea pande za Mombasa nchini Kenya
wakati nyota huyo alipokuwa akirekodi video ya wimbo wake uitwao The Gal
Bladder ambapo vijana hao walikatisha shughuli nzima na kuanza
kumkimbiza Baby Madaha.
“Daah! Ilikuwa noma, ilikuwa usiku sasa wakati meneja wangu
akinielekeza matakwa ya video hiyo ambayo yalihitaji vijana wa mtaani,
ghafla wakatokea vijana wenyewe wa mtaani na kutaka kunibaka. Bahati
nzuri nilifanikiwa kutimua mbio na kuwazidi,” alisema Baby.