MSAANI MAARUFU "KELLY ROWLAND " KUTOKA MAREKANI AKIWA KATIKA MITAA YA UWANJA WA FISI MANZENSE KUJIONEA MWENYEWE JIJINI DAR-ES-SALAAM




Msanii maarufu wa Marekani Kelly Rowland, ametinga uwanja wa fisi Manzese Dar es salaam jana jioni baada ya kusikia sifa za maeneo hayo ya Uswahilini tangu akiwa USA. Msanii huyo ametua nchini kwa tiketi ya MTV kupitia taasisi yake inayojishughulisha na kampeni za kupambana na Ukwimwi (Staying AliveFoundation) ya nchini Marekani, Kelly akiwa balozi wake. Akiwa Uwanja wa Fisi, ambako kunasifika kwa ufuska wa kupindukia na rate kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wasichana wadogo, Kelly alitembelea NGO ya EYG (Elizabeth Youth Group) inayojishughulisha na kutoa misaada ya elimu ya HIV/AIDS, uchangudoa, ulevi pamoja na uvutaji bangi kwa vijana nchini.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger