Taarifa hiyo imetolewa wakati wingu zito likiwa
limegubika uwasilishaji wa ripoti ya kikosi kazi cha Serikali
kilichochunguza sakata la Sh315 bilioni zilizofichwa na Watanzania
katika mabenki nchini Uswisi.
Takwimu hizo zilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe.
Zitto alisema taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa
Tanzania inapoteza kila mwaka mapato hayo ambayo ni sawa na asilimia
tano ya Pato la Taifa kupitia uhamishaji huo haramu.
“Uhamishaji huu haramu wa fedha kupelekwa nje ya
nchi hufanywa kwa lengo la kukwepa kulipa kodi au wahusika kuepuka
kukamatwa na fedha walizopata kwa kupokea rushwa,” alisema Zitto.
Kamati hiyo imependekeza Bunge kutunga sheria
itakayodhibiti uhamishaji haramu au ufichaji wa fedha nje ya kwa lengo
la kuogopa kukamatwa na rushwa, kufanya ufisadi na kukwepa kodi.
Zitto alisema hayo ni moja ya maazimio
yaliyofikiwa katika mkutano wa 10 wa Jumuiya ya Kamati za Hesabu za
Serikali za Mabunge (Sadcopac) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(Sadc).
Alisema katika mkutano huo uliofanyika Septemba 2
hadi 7, mwaka huu Jijini Arusha, wajumbe waliazimia kuhamasisha mabunge
ya nchi zao kutunga sheria kudhibiti uhamishaji huo wa fedha.
Wiki iliyopita, mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina
(CCM), alikaririwa akisema bungeni ‘hapatatosha’ kama ripoti ya
mabilioni ya Uswisi haitawasilishwa katika Bunge hili.
Mpina alisema yeye ni miongoni mwa wabunge
waliohojiwa baada ya kutamka bungeni kuwa zaidi ya Sh11.9 trilioni
zimetoroshwa kutoka Tanzania kati ya mwaka 1970 na mwaka 2008.
“Nilipolisema hilo jambo niliikabidhi Serikali
kupitia Bunge taarifa za tafiti mbalimbali ili ifuatilie. Baadaye Zitto
akaja na hoja ya bilioni 314… tunataka taarifa hatutanii,” alisema.
Ripoti hiyo ilikuwa iwasilishwe Bunge la Aprili
lakini Serikali ikaomba muda zaidi na kuahidi kuiwasilisha katika
Mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea Mjini Dodoma.
----Mwananchi
----Mwananchi