| ||
Bibi Lucia alivyokatwa panga |
Mama
mmoja aliyetajwa kwa jina la Lucia Mgonga (55) mkazi wa kijiji cha Mega
wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuwawa kwa kukatwa Mapanga na watu
wasiojulikana.
Tukio
hilo la kutisha limetokea Usiku wa kuamkia juzi majira ya saa mbili
usiku wakati bibi huyo akiwa na wajukuu zake wakipata chakula cha jioni.
Marehemu akiwa katika eneo alilokuwa akila chakula na wajukuu zake |
Marehemu amepoteza maisha baada ya kukatwa panga sehemu ya bega lake la kushoto na Shingoni.
Sababu ya mauwaji hayo inaelezwa kuwa ni imani za kishirikina.