Mwili wa jambazi hilo ukiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama |
Kijana mmoja ambaye hajatambulika
jina lake mwenye umri kati ya miaka 26 hadi 30 ameuawa kwa kupigwa risasi
wakati akiwa na wenzake wakijaribu kuvunja duka maeneo ya Shunu, kata ya
Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea majira ya saa
nane usiku wa kuamkia leo ambapo jambazi hilo likiwa na wenzake watatu liliuawa
kwa kupigwa risasi kichwani na Wilson Masolwa (63) mkazi wa mtaa huo ambaye
alijeruhiwa kwa mapanga.
Mtu huyo ameuawa kwa Bunduki aina ya
Shortgun ambayo hata hivyo wenzake waliipora baada ya kumkata mapanga Masolwa
na kupoteza fahamu.
Akizungumzia tukio hilo mmiliki wa
nyumba hiyo Yasinta Patrick (32) amesema mtu huyo na wenzake walivamia katika
nyumba yake, ambayo ameipangisha kwa wafanyabiashara wawili wa kutoa na kutuma
fedha kwa njia ya mtandao.
Mmiliki wa nyumba iliyovamiwa Bi Yasinya Patrick |
Kwa upande wake Masolwa amesema
baada kusikia kelele alifika katika eneo la tukio na ndipo majambazi hao
walianza kumkata mapanga kabla ya yeye kumpiga risasi ya kichwa mmoja wao na kufariki
dunia papo hapo.
Mzee Masolwa alivyojeruhiwa wakati akipambana na majambazi hayo |
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba Masolwa amefikishwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama kupatiwa
matibabu na kuruhusiwa na kwamba hali yake inaendelea vizuri.
Kamanda Kihenya mwili wa marehemu
huyo umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahamaa na kwamba jeshi la
polisi linaendelea na msako wa kuwabaini na kuwakamata wahusika watatu
waliotoroka ikiwa ni pamoja na bunduki waliyoipora.
Maduka yaliyokuwa yakifanyiwa uhalifu na majambazi hayo |
Mzee Masolwa |