David Moyes alionekana kwenye dimba la Vicente Calderon kwenye mchezo wa Atletico Madrid dhidi ya Porto usiku wa jana.
Kocha huyo wa Manchester United anategemewa kufanya usajili wakati dirisha la usajili mwezi ujao litakapofunguliwa baada ya kuwa na mwanzo mbovu.
Huku Atletico nao wakiwa wamefuzu wakiwa hajafungwa na wakiongoza kundi lao, Moyes inawezekana
hakuwa uwanjani pale
kuangalia timu ambayo anaweza kukutana nayo raundi inayofuatia, kiungo
wa klabu ya Atletico Koke anatajwa kuwepo kwenye rada ya Man United na
usiku wa jana ilifahamika wazi kwamba kiungo huyo ana kipengele
kinachoweza kumruhusu kuuzwa endapo tu klabu italipa kiasi kisichopungua
€24m.Hata
hivyo, mkurugenzi wa michezo wa Atletico Madrid, Caminero, haamini
kwamba Moyes alikuwa uwanjani pale kwa ajili ya kumfuatilia Koke.
“Inawezekana David Moyes alikuja hapa kuja kuangalia moja timu ambazo anaweza kukutana nazo mbeleni katika Champions League. Tumeonana na David, tumeongea lakini hakuniambia hasa kilichomleta hapa."
“Inawezekana David Moyes alikuja hapa kuja kuangalia moja timu ambazo anaweza kukutana nazo mbeleni katika Champions League. Tumeonana na David, tumeongea lakini hakuniambia hasa kilichomleta hapa."