HATIMAYE NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZATUMIWA NA UMOJA WA MATAIFA HUKO DRC KUPAMBANA NA M23


Majeshi ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yameanza kutumia ndege zisizo rubani kuchunguza harakati za waasi katika mipaka na Rwanda na Uganda. Hii ni mara ya kwanza kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa kutumia ndege za aina hiyo.
Ndege mbili za kwanza zilirushwa kutoka mji wa mashariki wa Goma ambao mwaka jana ulikaliwa kwa muda mfupi na waaasi wa kundi la M23.

Ndege mbili za kwanza zinaundwa na shirika la Italia la Selex ES.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kulinda amani Herve Ladsous ameiambia BBC kuwa ndege hizo zisizo na rubani, zitatumika kama njia mojawapo ya kufuatilia harakati za makundi yenye silaha na mienendo ya raia katika eneo la mashariki mwa Congo.
“Tunatakiwa kuwa na picha halisi ya kile kinachotokea,” amesema.
Amesema kama watafanikiwa nchini DR Congo, ndege hizo zinaweza pia kutumika katika maeneo mengine ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.
Source Bbc swahili.

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger