Mchezo kati Atletico PR na Vasco da Gama, ulisimamishwa Jumapili baada ya mashabiki kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe. Mashabiki waliokuwa wanapigana ilibidi watenganishwe na Polisi wa kutuliza ghasia kwa kuwafyatulia mabomu.
Mchezo huo ukaanza tena baada ya saa moja na dakika 10 za kusimama kupisha vurumai.
Tukio hili ni baya kwa Brazil, na litaifanya nchi hiyo ijipange kwa matukio ya aina hiyo wakati wa Fainali za Kombe la Dunia.
Mashabiki waliojeruhiwa wakibebwa kupelekwa kwenye helikopta