Taarifa hii ni kwa mujibu wa taasisi mbili za utafiti barani Afrika.
Hata hivyo wakati mwingi, al-Shabab ilisisitiza kusambaza chakula wenyewe na wakati mwingine hata kukichua badala ya kuwapa watu waliokuwa wanakumbwa na njaa.
Baadhi ya mashirika hayo yangali yanalipa Al Shabaab ili yaruhusiwe kuingi katika maeneo ambayo watu wanahitaji msaada nchini Somalia na hasa maeneo ambayo bado kundi hilo linadhibiti.
Zaidi ya watu 250,000 walifariki wakati wa janga hilo mwaka 2011.
Ripoti hiyo iliyotolewa na taasisi ya kimataifa ya maendeleo na ustawi pamoja na taasisi nyingine ya sera mjini Mogadishu, ilitaja pesa hizo kama malipo ya usajili na mashirika hutozwa hadi dola 10,000 za kimarekani.
Taasisi hizo zinasema kuwa wakati mwingine al-Shabab ilichukua chakula kilichonuiwa kupelekewa watu kama msaada katika mji wa Baidoa,