Mdau
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Madawa ya Kulevya
na Uhalifu(UNODC), Dkt. Edwin Swai akitoa Salaam katika Maadhimisho ya
Siku ya UKIMWI Magerezani yalifanyika leo Desemba 14, 2013 ndani ya
Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam(wa kwanza kushoto) ni Mdau kutoka Tume
ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Jumanne Issango na wa pili
kushoto ni Mdau kutoka Mpango wa Taifa wa Kuthibiti UKIMWI(NACP), Dkt.
Patrick Mwidunda.
Kikundi
cha Wasanii wa Mziki wa Kizazi kipya cha Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga
wakitumbuiza mbele ya Mgeni Rasmi( hayupo pichani) katika Maadhimisho ya
Siku ya UKIMWI Magerezani yaliyofanyika leo Desemba 14, 2014 ndani ya
Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam. Kikundi hicho kinaongozwa na Msanii
Papii Kocha( wa tatu kulia)ambaye anatumikia kifungo chake Gerezani.
Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikabidhi cheti
Maalum kwa Mmoja wa Wafungwa Waelimishaji rika kuhusu masuala ya UKIMWI
na Kifua Kikuu Magerezani leo Desemba 14, 2013 katika Maadhimisho ya
UKIMWI Magerezani ambayo yamefanyika ndani ya Gereza Kuu Ukonga.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba fupi ya Maadhimisho ya UKIMWI Magerezani leo Desemba 14, 2013 kwa Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam( hawapo pichani)
Wafungwa Waandishi wa Habari wa kujitegemea wa Shirika la Habari la Utangazaji la Taifa(TBC1) hawakuwa nyuma katika kuchukua matukio muhimu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Magerezani yaliyofanyika Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam leo Desemba 14, 2013