MALIMWENGU: WANAUME WAWILI MASHOGA WAPATA VYEO VIKUBWA SEREKALINI...MMOJA NI WAZIRI MKUU MWINGINE MSAIDIZI
Hii itakua ya kwanza duniani kwa wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kupata vyeo vikubwa kwenye serikali kuu ya nchi.
Makundi mengi yenye maoni tofauti yamekuwa yakipinga mapenzi ya jinsia moja na makundi mengine yakitetea, huko Luxemburg mwanaume anayejulikana kwa jina Xavier Bettel ambaye ameweka wazi kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja amekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.
Hapo hapo mwanaume mwingine Etienne Schneider ambaye pia aliweka wazi kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja amepewa umakamo waziri mkuu akimsaidia kazi Xavier Bettel .
Baada ya wawili hawa kupata vyeo hivi vya juu imefanya nchi ya Luxemburg kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na viongozi wa juu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja waziwazi.