PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili katika mji mkuu wa Afrika Kusini wa Pretoria usiku wa leo, Jumatatu, Desemba 9, 2013, kuhudhuria Ibada Kuu ya Kitaifa (Memorial Service) ya msiba wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg.
Rais Kikwete anajiunga na mamia ya viongozi wa nchi mbali mbali duniani kuomboleza kifo cha mmoja wa viongozi mashuhuri zaidi duniani katika karne za 20 na 21.
Rais Kikwete ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na mkewe Mama Asha; Mama Salma Kikwete na Ndugu Abdulahramani Kinana, Katibu wa Mkuu wa CCM