Bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari ya Lupata wakiwa wanashuhudia Jinsi bweni hilo likiwaka moto kwa kasi huku wengine wakiwa wanaendelea kuzima.
Mwenye Ndoo Hayaaa... Mwenye Mchanga hayaa .. walio simama hayaa.. hii ilikuwa ni kazi ya kufanya uokozi wa Bweni hilo ...
Hivi ndivyo Moto ulivyokuwa unazidi kuwaka huku wakifanya juhudi za kuzima moto huo, ambao ulikuwa unawaka kwa kasi.
Vijana wakiwa wanafanikiwa zoezi la kuzima moto huo huku kila mmoja akiwa anaongeza juhudi za kuzima Bweni hilo.
Tukio
Hili la kusikitisha lilitokea tarehe 29.10.2013 Katika Halmashauri
mpya ya Busikelo Wilayani Rungwe, ambapo Bweni hilo liliwaka Moto
mkubwa na kusababisha uharibifu wa Mali za wanafunzi na shule kwa
ujumla .