Mbunge Mch, Msigwa akanusha tuhuma nzito dhidi yake.....

1454628_602438129803504_1373062112_n_ed4ef.jpg
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha CHADEMA Mch Peter Msigwa amekanusha kuhusiana na tuhuma zinazomkabili juu ya kutokabidhi rambirambi kiasi cha shilingi milioni moja kwa mjane wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi, ambazo zilitolewa na wanachama wa CHADEMA waliopo nchini Uingereza na kusema kuwa tuhuma hizo si za kweli, ni mambo ya uzushi na kwamba watu wanasema hivyo ili kumchafua.
akizungumza na kituo cha redio ya Nuru FM ya Iringa, kupitia kipindi cha sunrise power, Mh.Msingwa amesema kuwa ni kweli pesa hizo alipokea kupitia kwa MAJID MJENGWA na baada ya kupokea fedha hizo alichangisha tena fedha kwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini kupitia mkutano, ambapo walichangia kiasi cha shilingi laki tatu pamoja na yeye mwenyewe aliongezea kiasi cha shilingi laki tano, hivyo kupelekea kufikia kiasi cha shilingi milioni moja na laki nane na sitini na nane na kumkabidhi mjane wa marehemu DAUDI MWANGOSI.
Msigwa amesema kuwa ni wanasiasa tu wanaojaribu kuwachafua baada ya kuona kuwa wameshindwa na tayari amewasiliana na uongozi wa chama chake ili kuweza kulichukulia hatua gazeti ambalo limeandika tuhuma hiyo

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger