RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR

Jakaya-Mrisho-Kikwete_5bcd9.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Johari Masoud Sururu kuwa Kamishna mpya wa Uhamiaji Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huu ambao unaanzia tarehe 24 Novemba, 2013 Bwana Sururu alikuwa Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania jijini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).
Kufuatana na uteuzi huu, aliyekuwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Bwana Mwinchumu Hassan Salim sasa atapangiwa kazi nyingine.
Imetolewa na:
Isaac J. Nantanga
MSEMAJI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
04 Desemba, 2013

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger