Pendekezo hilo ni hatua ya awali katika juhudi za kurejesha utawala wa kidemokrasia baada ya kutimuliwa mwezi Julai kwa rais Mohamed Morsi. Pia itachukua nafasi ya katiba yenye utata iliyoidhinishwa na rais wa Kiislam Morsi.
Katiba mpya inataka uchaguzi wa rais na bunge kufanyika ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya wapiga kura kuipitisha.
Lakini itakuwa ni chaguo la rais wa mpito Adly Mansour kuamua ikiwa uchaguzi utafanyika kwanza