MWENYEKITI WA NEC ATOA UFAFANUZI KUWA TUME IKO HURU

unnamed_2581b.jpg
Na Magreth Kinabo
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian Libuva ametoa ufafanuzi kuwa tume hiyo iko huru na si kweli kwamba haiko huru kama inavyonukuliwa katika baadhi ya taarifa na watu .
Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Lubuva wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC jijini Dares Salaam, alisema tume hiyo iliundwa kwa mujibu wa sheria kupitia Iba
Jaji Libuva alisema kwa muda mrefu katika chaguzi mbalimbali yamekuwepo mlalamiko dhidi ya tume kuwa si huru na moja ya sababu zinazotolewa ni kutokana na mfumo wa uteuzi wa makamishina wa tume kuchaguliwa na Rais, ambaye ni kiongozi wa Chama tawala.
" Hili linapigiwa kelele hasa na vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi. Mara kadhaa katika mijadala limerudiwa rudiwa na hata baadhi ya vyombo vya habari vimenukuliwa vikisema hata Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amekiri kuwa tume siyo huru.(P.T)
Tume inafanya kazi zake za kusimamamia na kuongoza shughuli za uchaguzi kwa uhuru ,na wazi bila kuingiliwa na chombo chochote iwe ni seriklai au Chama chochote cha siasa," alisema Jaji Lubuva.
Aliongeza kuwa tume hiyo haijawahi kuagizwa kuendesha uchaguzi kwa kupendelea chama au mgombea yeyote.
Aidha alisema katika mihadahra ambayo tume hiyo ilialikwa msimamo wa umekuwa ukitolewa ni Tume Huru.
" Nimetoa mada katika vyuo vikuu Iringa na Dares Salaam ambapo uhuru wa Tume umehojiwa katika mada hizo nimesisitiza juu ya suala hilo," alisisitiza .
Jaji Lubuva alifafanua kuwa kwa vile mfumo uliopo wa tume hiyo ni wa Kikatiba, kama wananchi na wadau kwa ujumla wanataka mfumo wa uteuzi wa wajumbe wa tume ubadilike , basi wachukue fursa hiyo kutoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

pop up

 
Support : KARIBU TENA BONGO MASKANI
Copyright © 2011. BONGO MASKANI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA BONGO MASKANI
Proudly powered by Blogger