TANZANIA YAKUSANYA POINTI TATU LEO DHIDI YA SOMALIA KOMBE LA CHALLENGE HUKO KENYA
Baada ya timu ya soka ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Ethiopia katika mechi ya michuano ya Kombe la Chalenji iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi.
Timu ya soka ya Tanzania bara,Kilimanjaro Stars leo imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Somalia.
Bao pekee la Haroun Chanongo dakika ya 57 limetosha kuipa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Somalia mchana wa leo katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Hivi sasa Kilimanjaro ina pointi nne baada ya kufungana bao 1-1 na Zambia kwenye mechi iliyopita na ushindi wa 1-0 dhidi ya Somaria wakati Somalia haina pointi baada ya kupoteza mechi zake zote dhidi ya Burundi na Kilimanjaro stars.