Baadhi
ya Maseneta wa majimbo mbalimbali nchini Marekani wamekosoa kitendo cha
Rais wa nchi hiyo Barack Obama kupeana mkono na kiongozi wa Cuba Raul
Castro wakati wa kumuaga mzee Nelson Mandela Johannesburg South Africa.
Mmoja
wao ambae ni Bi Lehtinen amesema ‘wakati kiongozi wa ulimwengu huru
anaposhikana mkono na kiongozi ambae ni dikteta inaonekana wazi kabisa
kwamba hili ni tukio lililopangwa, Raul Castro anatumia mkono huu huu
kutia saini maamuzi ya kikatili yanayokandamiza, kunyanyasa hata watu
wasio na hatia’
‘Hivi
tunavyozungumza Viongozi wa Upinzani Cuba wanakatwa na kuteswa kwa
kupigwa bila hatia, wanafungwa gerezani na kufanyiwa mengine ya kikatili
kupitia ruhusa ya mkono huohuo wa alioshikana nao Rais Obama’ –
Lehtinen.
Pamoja
na kushikana mkono na Raul, Rais Obama kwenye hotuba yake aliyoitoa
muda mfupi baadae alionekana kumpa madongo Raul kwa kuwaponda
wanaomlilia Mzee Mandela wakati wao wenyewe wanashindwa kutekeleza yale
mazuri aliyokua akiyafanya ikiwemo siasa za kistaarabu.
Wengine
waliopinga kitendo cha Rais Obama kumsalimia Raul kwa kupeana mikono ni
Seneta John McCain ambae amesema hiki kitendo ni sawa na kupeana mkono
na Adolf Hitler na kusisitiza ‘kwa nini upeane mkono na mtu ambae bado
anawashikilia Wamarekani kwenye magereza yake?’