Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar, Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Sepetu imetolewa hukumu yake baada ya Wema kuomba iharakishwe kwakuwa alikuwa anasafari.
Kwa mujibu wa mtandao wa Global Publishers, Wema sepetu amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu gerezani ama faini ya shilingi laki moja kwa maana ya elfu hamsini kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo mawili ya kupiga na kutukana.
Baada ya kusomewa hukumu hiyo wema alitoa laki moja hiyo iliyokuwa ikihitajiwa na mahakama kabla ya kuachiwa huru kuendelea na mishe zake nyingine