WENYEJI
Kenya, Harambee Stars wameanza vibaya Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kulazimishwa sare ya bila
kufungana na Ethiopia katika mchezo wa Kundi A, Uwanja wa Nyayo,
Nairobi, Kenya.
Ethiopia waliitesa Kenya kwa soka ya ‘Kibarcelona’, huku wachezaji wa Harambee wakitumia nguvu zaidi na maarifa haba.
Bao la Sudan Kusini lilifungwa na Fabiano Lako dakika ya 73, zikiwa ni dakika tano aiingie kuchukua nafasi ya Francis Khamis.
Kikosi cha Kenya kilikuwa;
Duncan Ochieng, David Ochieng, Mussa Mohamed, Aboud
Omar, Joackins Atudo/David King’atua k73, Peter Opiyo, Francis Kahata,
Anthony Akumu, David Gateri, Edwin Lavatisa na Allan Wanga.
Ethiopia;
Derete Alemu, Fasika Asfan, Salahadin Bargicho, Thok James, Moges
Tedese, Shemeless Tegne, Mulualem Mesfin, Mintesnote Adane, Yussuf
Yassin/Shimekit Gogsa dk89, Gebremichael Yakob/Yonathan Kebede dk46 na
Foad Abbas/Manaye Fantu dk46.
ZANZIBAR YAANZA VYEMA CHALLENGE, YAICHAPA SUDAN KUSINI 2-1
Matokeo
hayo yanaifanya Zanzibar iliyoshinda 2-1 mchezo wake wa kwanza dhidi ya
Sudan Kusini iongoze Kundi na kujiweka katika mazingira mazuri ya
kuingia Robo Fainali.
Zanzibar ingeweza kuondoka na ushindi mnene leo kama washambuliaji wake, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Ally Badru wangetumia vyema nafasi nzuri walizopata. Nafasi nzuri zaidi ambayo Zanzibar walipata ilikuwa dakika ya 43 baada ya Badru kumlamba chenga kipa, lakini Khamis Mcha alipopiga pira ukagonga mwamba na kipa akaudaka.
Zanzibar;
Zanzibar ingeweza kuondoka na ushindi mnene leo kama washambuliaji wake, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Ally Badru wangetumia vyema nafasi nzuri walizopata. Nafasi nzuri zaidi ambayo Zanzibar walipata ilikuwa dakika ya 43 baada ya Badru kumlamba chenga kipa, lakini Khamis Mcha alipopiga pira ukagonga mwamba na kipa akaudaka.
Zanzibar;
Abdallah Rashid, Salum Khamis/Ally Khan dk78, Waziri Salum, Shaffi
Hassan, Mohamed Fakhi, Sabri Ali, Masoud Ali, Suleiman Kassim, Awadh
Juma na Khamis Mcha/Amour Omar dk44/Adeyoum Saleh dk62.
Sudan Kusini;
Sudan Kusini;
Juma Jinaro, Atar Thomas, Philip Delfino, Edomon Amadeo,
Richard Justin, Wiiam Offiri, Jimmy Erasto, Thomas Jacob, Godfrey Peter,
Francis Khamis/Fabiano Lako dk68 na James Joseph.
Michuano
hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili huko Machakos, Tanzania Bara
ikimenyana na Zambia jioni baada ya Somalia na Burundi kupepetana
mchana.